Mwalimu Nyerere na Maadui 3, Nyufa 3

Mwalimu Nyerere na Maadui 3, Nyufa 3

Msittu

Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
7
Reaction score
36
Tathimini binafsi ya Baba wa Taifa ilijikita katika uzoefu alioupata kifalsafa, kiutawala na kiuongozi. Mwalimu alianza kwa kutabanaisha kuwa ili Tanzania ipate maendeleo ni sharti kuwakabiri maadui watatu: Umasikini, Ujinga na Maradhi.

Katika kutambua ugumu na mwelekeo wa vita hiyo, Mwalimu aliona mtikisiko katika Taifa uliozaa nyufa tatu: Rushwa, Muungano na Katiba.

Kwa bahati nzuri utatuzi wa masuala hayo Mwalimu aliuweka bayana kuwa ni lazima kuwe na Siasa safi, Uongozi bora, Ardhi na Watu.

Sina shaka haya mambo yapo bayana kwa Umma. Huu ni mtego wa Umma, ni mapinduzi pekee yanayoweza kuleta mabadiliko. Mwalimu aliamini katika mapinduzi ya fikra, aliamini njia salama ni kupitia fikra pingani.

Mawazo na maarifa ni lazima yasigane kujenga misingi imara.
 
Adui namba moja alikuwa yeye mwenyewe alichomfanyia Kambona kwa sababu ya kutofautiana mawazo tu anajua yeye pamoja na wanaojua historia ya nchi hii. Alitupandia mbegu mbaya mpaka leo inatutesa na ukitaka kuiona nchi hii chungu wewe tofautiana tu mtizamo na watawala
 
Mkuu unisamehe mwacha Mwl apumuzike huko,usipoteze muda wako na misemo ya Mwalimu.
Alianza vizuri akisema katika kimombo:It can be done play your part,kuhusu maadui watatu yaani Ujinga,Maradhi,Umaskini.
Na hiyo ndio miaka michache ya mwanzo,ambako tulikuwa tuna misingi ya kufanya kazi kama alivyotuachia mkoloni tukiwajibika kwa wananchi period.

Lakini mara baada ya kuanzisha AFRICANIZATION akiwandoa wazungu,na wageni kwenye nafasi zao na kuwaajiri wana Tanu wengi wao wasio na sifa za kazi kwa upendeleo, ndio magonjwa ya rushwa,uzembe,yalipoibuka kwa nguvu.

Ili kuzima mtafaruku ulioukijitokeza mara kwa mara kutokea vyama vya upinzani hasa ANC ikiongozwa na Zuberi Mtemvu walihoji uhalali wa madudu yaliokuwa yanafanywa na serikali ya Tanu. Badala ya kujisahihisha Dr.Julius Kambarage Nyerere akaja na mikakati kuuwa kwanza Multiparty ili kuuwa kabisa vyama pinzani, kuuwa Local goverment ,kufidhoofisha vyama vya Ushirika.

Baadae silaha ilikuwa imebakia ilikuwa Elimu,ebu jiulize kwanini wanafunzi wa Mlimani waliandamana hadi Ikulu wakisema AFADHALI YA MKOLONI?unadhani walikuwa hawajui wanadai nini?
Ili kumaliza kabisa upinzani wa wasomi ilikuwa mpango kamambe ambao hadi leo unatugharimu.
Kuvunja nguvu ya communication skills mashuleni akaondoa English
Shule za taasisi za dini zikatwaliwa na serikali.
Syllabus za masomo zikajaa siasa za mwalimu
UPE
Musoma Resolution
N,k

Mkuu mimi siko pale kutengua mawazo yako,ila mimi kwa mawazo yangu naona tunazunguka zunguka,tunajua nani alihujumu maendeleo ya nchi kwa kutetea maslahi yake binafsi ya kuwa kiongozi bila kupingwa kwa miaka mingi.
 
Mwalimu alikuwa binadamu hakuwa malaika. Hapo kwanza naomba tuelewane kuna wakati alitoka kwenye njia sahihi kwa sababu zake binafsi unaweza ukatuambia ni kosa gani alifanya Kambona mpaka akapewa kesi ya uhaini? Alale mahala pema Mwalimu lakini kuna maeneo na yeye aliyakologa sema yeye alikuwa mwepesi wakusoma nyakati alipoona sera zake zimegonga mwamba alikaa pembeni kukwepa lawama
 
Nakumbuka kuna wakati lawama zilimwendea Rashid Mfaume Kawawa,wakati mtoa maagizo mabovu alikuwa mwenyewe Mwalimu Nyerere.
Kawawa alikuwa hataki mapambano na Mwl.akageuzwa punching bag ya Mwl.lakini kwa watu tuliowahi kufanya na Mzee Kawawa alikuwa kiongozi hodari.ndio siri ya kuitwa simba wa vita.
 
Kuna wakati Mwalimu alikuwa wrong kwenye mipango yake ila kwa mboni ya kawaida huwezi kujua
 
Back
Top Bottom