Mwalimu amvunja mwanafunzi mkono kwa adhabu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
270
Mwalimu amvunja mkono mwanafunzi wake

Mwalimu wa Kiingereza katika Shule ya Msingi Furaha jijini Mwanza, Jafeth Manyirizu, anatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kufuatia kudaiwa kumvunja mkono mwanafunzi wake, Asia Yasini, wakati akimwadhibu kwa kumpiga kwa ubao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Siro, chanzo cha mwalimu kumvunja mkono mwanafunzi huyo ni kupindisha mstari wakati akifundishwa somo hilo. “Jeshi langu linaendelea na upelelezi wa tukio hili ili liweze kumtia katika nguvu za dola na sheria iweze kuchukua mkondo wake dhidi iya mwalimu huyu katili,” alisema Siro ambaye amewaomba Walimu wenye tabia hiyo kuacha vitendo hivyo kwani kitendo alichofanyiwa binti huyo ni cha ukatili.

Mkuu wa shule hiyo, Emmanuel Manoni, amesema hana taarifa za kitendo alichofanya Mwalimu huyo lakini akaahidi kuwa atazifuatilia ili kuzifahamu kwa undani.
 
Huyo mwalimu atakuwa na mambo ya kizamani ya kupiga watoto. Watoto wa siku hizi unaongea nao ukishindwa unawapa adhabu. Mambo ya kupiga yalishapitwa na wakati. Achukuliwe hatua za kisheria tu.
 
Tabia hii ya kuchapa na ku-abuse watoto shuleni na waalimu ikome kabisa, it violence against children's rights? Kwani ukimpiga mtoto au kumpindisha mkono ndio akili inakuja? Kwanza kwa mtoto kushindwa jambo pia inawezekana ni udhaifu wa mwalimu, a student's failure is not his/her alone....walimu acheni hiyo abuse. Mtashtakiwa na wengine tunaotetea haki za watoto tuko tayari hata kutoa huduma za bure za advocacy; you will rot in jail. And I pray the idiot teacher who hurt that kid will face the full terror of the law....mshenzi sana, "sina adhabu"
 
Back
Top Bottom