Mwakyembe: Nani Amekuloga?

Prince Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
910
Reaction score
247
Dr H. Makyembe miaka michache tu iliyopita alikuwa ana haiba, heshima,ushujaa na uzalendo ndani na nje ya bunge ambao watanzania nadhani bado tunakumbuka.

Tume yake iliyompukutisha Edward Lowasa na Governer wa BOT kipindi hicho bwana Balali,aliye-assume amefariki dunia ( yupo hai) ni baadhi ya matunda ya uzalendo wake. Hakika kipindi hicho alikuwa NURU ndani CCM, hakuwa shabiki wa chama lakini alisimamia ukweli alioamini japo hakupendwa na wabunge karibu wote ndani ya CCM kwa kazi yake.

Mwakyembe yule...Sio huyu tulienae, AMELOGWA NA NANI?. Tuamini kwamba alikuwa hivo kwa maslahi ya taifa na sasa yuko kwa maslahi ya chama chake CCM?..

Tuamini kwamba wabunge wa CCM hawatetei tena maslahi ya taifa bali CCM? Ni kwa nini hatowi cheche zake dhidi ya fedha zetu zilizoko Uswiss? Hajasikia kwamba Tembo wanakwisha kwenye hifadhi kwa ujangili wa kinana?

Haoni kazi wanayofanya Filikunjombe na Kangi Lugola?

A
seme aliyemloga (alitishwa? Kule kupewa uwaziri? Alipata alichokuwa anahitaji?).

Kweli amelogwa.
 
Wewe kweli ni mtu mjinga sana.
Serikali yoyote duniani huongozwa na collective responsibility katika maamuzi, hata kama hukubakiani nayo.
Ndani ya uongozi wa serikali hakuna one-mans-show, kama ilivyo ndani ya vyama kama Dr Slaa na CHADEMA yake.

Ukisha elewa hilo mengine utajijibu.
 

Already you are defeated! Those led by emotions than reasoning are totally boxes headed...come with resoning, you are a role model of poor thinkers...teh..teh..teh..teh
 

Dr. Mwakyembe hajalogwa kama unavyodhani bali kanuni zinambana kutoihoji serikali wakati yeye ni sehemu ya serikali, wakati unaousema wewe alikuwa ni mbunge na kazi ya mbunge ni kuhoji, kukosoa na kuikemea serikali ndiyo maana alifanya hayo yaliyokufurahisha. Kifupi ni kwamba Waziri hana ruhusa kuishambulia serikali.
 

Ndugu yangu kinachokusumbua wewe ni uelewa wako mdogo juu ya kazi na majukumu ya Mbunge na kazi na majukumu ya Waziri.
Dr. Mwakyembe hajalogwa kama unavyodhani bali kanuni zinambana kutoihoji serikali wakati yeye ni sehemu ya serikali, wakati unaousema wewe alikuwa ni mbunge na kazi ya mbunge ni kuhoji, kukosoa na kuikemea serikali ndiyo maana alifanya hayo yalikufurahisha. Kifupi ni kwamba Waziri hana ruhusa kuishambulia serikali. HUKO ALIKO HUONI ANACHOKIFANYA?
 
I see!!...
Na Samwel Sita aliyekuwa anawapotosha Tanesco wasiilipe Dowans yupo kwenye Seikali ya Dr Slaa!? akili matope kabisa.
 

It doesnt sound low!...ana fulsa ya kuishauri serikali even outside yhe parliament.....so uozo anauona,nchi inaenda kombo then he is within the web...in the same box
 
Hivi hizo kanuni haziwabani mawaziri wengine? Mbona naambiwa wapo mawaziri wanawatetea mafisadi na majangili? Oops, sorry...ni collective responsibility!
 
Previously nilikuwa namkubali huyu mchizi lakini nilikuja kugundua ni mfia tumbo kama sendeka, zile mbilinge zote za richmond kumbe alikuwa anatafuta uwaziri. angekuwa na integrity hata punje moja asingekubali kuingia kwenye hii corrupt cabinet, trust no one.
 
Already you are defeated! Those led by emotions than reasoning are totally boxes headed...come with resoning, you are a role model of poor thinkers...teh..teh..teh..teh
Duhu aisee Prince tumbo, kwani kuandika kwa Kiswahili imekuwa ni adhabu? Si afadhali tu utumie lugha ya taifa badala ya kuchakachua lugha za wengine. Tutakuelewa vile vile, tena sana.
 
Last edited by a moderator:

Mhukumu mtu kwa majukumu yake mkuu, naamini unaijua kwa sasa yeye ni waziri na anafanya nin i huko, sasa hayo mambo yote ukitaka afanye yeye tu nadhani utakuwa humtendei haki. inchi hii inawatu wengi inatakiwa na cc tuwaunge mkono wanaonyesha njia baadala ya kuwalundikia mizigo ya majukumu.

Hata huyo Filikunjombe kesho aking'olewa kucha na meno na sirikali hatutaona watu wakichukua hatua yeyote japo wanajua kila kitu kuhusu hayo zaidi ya kuishia kusimuliana mtaani. tuwaelimishe watanzania wafanye mabadiliko kupitia sanduku la kupigia kura.

Ikumbukwe tatizo tulilonalo ni mfumo uliopo so hata mwakyembe angejitolea uhai wake bado hawezi kutatua hayo matatizo.
 
Duhu aisee Prince tumbo, kwani kuandika kwa Kiswahili imekuwa ni adhabu? Si afadhali tu utumie lugha ya taifa badala ya kuchakachua lugha za wengine. Tutakuelewa vile vile, tena sana.
Mkuu Askari Kanzu labda hajuwi kuandika lugha ya Taifa ndio maana kachakachuwa kuandika kimombo tehtetehteh
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Askari Kanzu labda hajuwi kuandika lugha ya Taifa ndio maana kachakachuwa kuandika kimombo tehtetehteh

Mkuu yaani wakoloni walitufanya kitu kibaya sana yaani watu wanadhani wakichangia kwa kiingereza ndo ataonyesha kwamba anajua vitu.

na hili suala linaanzia kwa rahisi wetu Jk cku amekuja rais wa china mwenzake anaongea lugha yake yeye anapiga kimombo. na Membe naye cku amekuja kibaki yaani kibaki anaongea kiswahili yeye anapiga kimombo.

Mungu atuepusha na huu utumwa wa fikra
 
Mkuu Open-Minded umenifurahisha yaani Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Mwai Kibaki anazungumza mlugha ya taifa Kiswahili wakati mwenyeji wake Waziri Membe anazungumza kimombo hahahahahah kasheshe kweli huo ni utumwa wa mambo leo kupenda kuzungumza lugha sio ya kwako wakatı mgeni wako anazungumza lugha ya kwako haya tutaendelea hivyo kwa kuiga mambo tusiyoyaweza.
 
Last edited by a moderator:
kweli kwko " battery low"... upiganaji wa Dr. H. M. hauoni? madudu bandari?, train Dar? mpaka wanamkoboa sura? jaribu kufikiria kuwa, " u can't eat ur cake and have it"...
 

Mkuu ndo maana viongozi wetu wamekuwa ombaomba sana kwa sababu wanatukuza vya wazungu wakati cc tunavyozaidi yao.
 
Sasa anakula kuku kwa mrija unadhani atawakumbuka hapo muhesabie gari limewaacha hii ndio tz
 
NA TOA OFA YA KWENDA KUCHUNGUZA MINYOO INAYO SHAMBULIA UBONGO. Maana hapa kuna vitu ukisoma una-diagnose kuwa ni Encephalitis, Neurocystercecosis +++++++++++.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…