Mwakyembe, Kipande wavurugana TPA

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,628
Reaction score
6,818
MIEZI sita baada ya Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe, kumteua Mhandisi Madeni Kipande, kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), viongozi hao kwa sasa hawaivi chungu kimoja, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Tofauti za viongozi hao imeelezwa kuwa ni baada ya Kipande kudaiwa kukaidi maagizo ya Waziri Mwakyembe.Habari ambazo gazeti hili limezipata, zilisema kuwa- Waziri Mwakyembe amemlima barua kali ya onyo Kipande, akimtaka kusitisha uamuzi wa kuibeba kampuni ya kuhifadhi magari ya SILVER.

Kampuni hiyo imekuwa ikilalamikiwa na kampuni nyingine kwamba inapendelewa na Kipande.

Barua hiyo ya Juni 11 ambayo nakala yake tunayo, Waziri Mwakyembe amembana Kipande kuacha kuipendelea kampuni hiyo.

Katika barua hiyo yenye kichwa cha habari: ‘Kukaidi maagizo ya wizara’, Dk. Mwakyembe alimtaka Kipande atakapojibu atumie kumbukumbu namba CCB 364/505/01.

Dk. Mwakyembe ameandika katika barua hiyo kuwa amepata taarifa ya kuwapo kwa upendeleo wa moja ya makampuni ya kuhifadhi magari kinyume cha maelekezo yake aliyoyatoa Machi 3, mwaka huu alipokutana na viongozi wa wizara na wawakilishi wa ICDSVS.

“Nimefedheheshwa sana na taarifa kuwa kampuni ya kuhifadhi magari ya SILVER bado inapata ‘preferential treatment’ au bado inabebwa na TPA tofauti na kampuni nyingine za aina hiyo na kinyume kabisa cha taratibu za ushindani na kibiashara na maelekezo niliyoyatoa mbele yenu viongozi wa wizara na wawakilishi wa ICDSVS tarehe 5, Machi 2013.

“Kwa staili hii ya uongozi hatufiki, sitisheni ‘preferential treatment’ kwa Silver ‘asap’ na nipate taarifa ya utekelezaji tarehe 15 Juni, 2013 bila kukosa,” imeandikwa barua hiyo.

Nakala ya barua hiyo imepelekwa kwa Profesa Joseph Msambichaka, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Bandar

Wakati Kipande akiandikiwa barua ya kusitisha uamuzi huo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa kaimu huyo amekuwa akilalamikiwa na makampuni tofauti hata nyingine kuamua kutoa notisi ya kukwepa kutumia Bandari ya Dar es Salaam na badala yake kuishia Mombasa.

Kikubwa kinachodaiwa na makampuni hayo kuamua kutoa notisi hiyo ni kukithiri kwa rushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kuwapo misuguano baina ya wafanyakazi wa bandari na wateja wakubwa wa ndani na nje ya nchi, hasa wenye meli.

Wateja wa ndani wanaodaiwa kulalamikia utendaji wa Kipande ni pamoja na Kampuni ya Tanga Cement, huku Kampuni ya Mesina kutoka nchini Italia ikielezwa kuwa tayari imeshatoa notisi ya kuacha kutumia Bandari ya Dar es Salaam na badala yake kuishia Mombasa nchini Kenya kutokana na ushirikiano mdogo inaodaiwa kutoka kwa Kipande.

Januari 21- mwaka huu- Waziri Dk.- Mwakyembe aliwatimua kazi vigogo watano wa bandari ambao ni Ephraim Mgawe, naibu wake, Hamad Konshuma, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Casian Nghamilo, Kapteni Tumaini Masalo na Julius Semfuko.

Vigogo hao walidaiwa kukutwa na makosa ya uzembe uliokithiri, kushindwa kudhibiti wizi, kukosa uaminifu kupindukia, matumizi mabaya ya madaraka na kukiuka sheria.

Wakati huo Mwakyembe alisema kuwa makosa hayo yamesababisha kushindwa kudhibiti kiwango cha utoaji mafuta machafu bandarini na kusababisha wizi wa mafuta masafi pamoja na kutoa kibali cha utoaji mafuta hayo kinyume cha sheria.

Waziri Mwakyembe aliongeza kuwa vigogo hao kwa kushirikiana walitumia vibaya madaraka yao kwa kuingia mkataba na kampuni ya Kichina (China Communication Construction Company) bila idhini ya serikali pamoja na kupandisha mshahara kwa wafanyakazi wa bodi hiyo bila idhini ya waziri anayesimamia mamlaka hiyo.Alisema kutokana na makosa hayo wameisababishia- Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya- mwisho kwa utendaji kati ya bandari 36 Afrika, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na DANIDA na Benki ya Dunia.

Wakati huo Dk. Mwakyembe alipofanya uamuzi huo na kumkaimisha Kipande katika nafasi ya ukurugenzi, taasisi mbalimbali za kimataifa zilionesha wasiwasi wao juu ya hali hiyo na kutahadharisha kuwa utaua uchumi wa nchi hasa katika sekta ya Bandari.

Taasisi zilizoonesha wasiwasi huo ni Umoja wa Ulaya (EU) na Benki ya Dunia (WB) ambazo kwa nyakati tofauti zilitoa maoni yao juu ya hali hiyo.

EU kwa upande wake ambayo ilifanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kusifia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ilihofia mafanikio hayo kupotea.

Tanzania Daima
 

Attachments

  • MOT.jpg
    138.2 KB · Views: 1,121
Hiyo Barua alitakiwa kuiambatanisha na zile zoote ambazo aliwalima akina Mgawe na wenzake...
 
Tanzania Daima bana,
Mbona hii ni barua ya kawaida kabisa kiutendaji ofisini. Sijaona mvulugano hapo kama gazeti linavyopenda IWE..

Hii ndiyo maana ya kuwa na mamlaka ya uongozi na usimamizi katika utendaji.

Hii barua inaonyesha ni jinsi gani waziri Mwakyembe asivyoweza kubeba watu ambao wanaenda nje ya utaratibu na sheria za kiutendaji hata kama ni rafiki zake au ndiye aliyewaweka katika ofisi.

Kukumbushwa wajibu na misingi ya kazi across department siyo jambo la ajabu labda huyo anayeona ajabu utendaji wake utakuwa based on nepotistic.

Inaeleweka Tanzania Daima liko desperate kwenye 'signed mission' za kisiasa mpaka habari zake kuhusu Mwakyembe zinakuwa a ki-machiavellian.
 
Wakuu hivi hii kitu inayoitwa Telegram inatumiwaje, nakumbuka niliwahi kusoma nikiwa darasa la tano shule ya msingi lakini sikuwahi kubahatika kuona ikitumika.
 
Big up Mwakyembe Tanzania inahitaji kiongozi kama wewe kwenye level ya uraisi ili iweze kuendelea na hivi huyo kipande amerogwa au? yaani Rushwa inamfanya aipotezee nchi wateja wa bandari kweli? Mwakyembe anapaswa kuiagiza PCCB kumchunguza lazima kutakua na rushwa tu hapo
 
Mwakyembe majuzi alikuwa UK moja ya vitu alivyovigusia alipokutana na wadau huko ni ziara yao ya Asia, unlike yule mama waziri aliekuja na city plan na kuisifia. Mwakeyembe alikuwa very impressed na jinsi bandari aliyoiona ni ndogo hila jinsi operation ilivyokuwa inafanyika si mchezo.

Kitu kikubwa ambacho kakiona au kajifunza huko(kwa mujibu wa madau) ni know-how na nasikia kakubali tatizo la kwanza ni huwezo wa human capital, ambapo bandarini kumejaa vilaza hilo pekee ni tatizo kubwa sana kufanya operation nazo ziwe mbovu. Ukichanganya na watu kama hawa sasa wasio angalia ubora wa tender na kuangalia maslahi dnio kabisa.

Katoa rai kwa watanzania ambao wapo qualified na wapo nje ya nchi kwenye wizara yake kazi watapata tu amekubali nyumbani bado, well atleast he was being honest (that is kama kweli mdau alimsikia akiyasema hayo).
 
Pamoja na kazi nzuri anayoifanya Waziri Mwakyembe......in my opinion hiyo barua imekaa kinafiki nafiki hivi.......ilitakiwa aandike.......Nataka maelezo/taarifa kuhusu mchakato mzima na tuhuma zifuatazo kuhusu SILVER........

Kuwaambie sitisheni....ni kulea UDHAIFU katika utendaji na maendelezo ya MAJUNGU...........
 
Sasa Kipande mbona ameanza njaa mapema?.Si angesubiri apewe u-DG kwanza?.Kwa namna hii,uteuzi wa TPA Management team mpya utachukua muda mrefu hadi Dr.Mwakyembe kukubali.
 
we jamaa barua si imeandikwa SIRI mbona umeianika hadharani? By the way big up sana Mwakyemango!
 
Bigup Dr! Usichike kuondoa watendaji dhaifu km hao, ambao wanapelekea serikali kuonekana dhaifu.
 
Kuna Rais mmoja wa Russia ambaye alifukuza sana mawaziri wakuu ambao alikua akiwateua mpaka alipotokea PUTIN...ambaye ameimarisha uchumi wa Russia mno...so Hongera Mhe. Mwakyembe endelea na Mungu akusaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…