BAADA ya kuwasimamisha kwa miezi kadhaa kupisha uchunguzi waziri wa uchukuzi Dakta Mwakyembe tangu ijumaa tarehe 24/5/2013 amewatimua kazi wakurugenzi wengine 3 na meneja 1 wa mamlaka ya bandari waliotimuliwa ni Bi Florence Nkya mkurugenzi mipango, Bi Maimuna Mrisha mkurugenzi mawasiliano, Injinia Bakari Kilo mkurugenzi ufundi na Edmund Swai meneja wa ujenzi.
hapo namba imekamilika kwani tayari alishawatimu wakurugenzi Efraim Mgawe,Ahmad Koshuma,Juliasi Mfuko na Kamti. kwa wakurugenzi wa zamani kabaki mpika majungu mkubwa nae anatakiwa kusambaratishwa pia ni mkurugenzi wa masoko mama Fransiska Kajumulo Muhindi[mdogo wake waziri mama Anna Tibaijuka]. Fransiska nae pia ameomba nafasi ya DG majuzi zilipotangazwa ni kituko kweli kweli. yuko likizo marekani.