Maoni yangu kwa Mwakyembe, pamoja na mauchunguzi yote yanayoendelea, fanya haya: TPA pamoja na TRL fanya recruitment upya! Kila mtu aombe ajira na utoe kwa masharti mapya ya kazi. Na hili liambatane na 'Performace agreement' kwamba kila mtu, kuanzia DG hadi secretary apewe target.
Kuna uozo mwingi sana TPA na TRL. Ukienda kwenye ofisi za TRL watu wako busy na mambo yao, hawataki kabisa kujishughulisha. Na ukiangalia kwa makini utagundua huyo mtu hana pressure - hana target anayotakiwa kufikia kwa hiyo apige domo au ale chapati yote sawa tu.
Ajiri upya- na weka masharti mapya.