Mwakyembe achana na TFF

MWAKATA KWETU

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
560
Reaction score
320
Nimefurahishwa sana na Raisi wa TFF kukaidi wito wa Waziri Mwakyembe,,
TFF ni taasisi huru,,haingiliwi na mtu yeyote nje ya sheria za Soka.
Kocha wa TAIFA alitafutwa na TFF ,,wao ndio wameona hajafiti kwenye hiyo nafasi.
Mwakyembe usituvuruge,,tuache tupange ya kwetu,,usije na hizo sheria zako....oooooh mara Simba na Yanga wamesajiri wachezaji wengi wa kigeni,,,
kwani wewe unatakaje???
Niipongeze TFF kwa kuanzisha Academy Dodoma ambayo itachukua watoto wenye vipaji vya soka na kuwalea....
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kiki zikizidi mwisho wa siku ni kuaibika tu.
 
Ni kweli TFF ni taasisi huru, ila ni mali ya serikali ya Tanzania. Huo uhuru unaousemea ni wa wapi?

Fifa pia walikua wakijidanganya wako huru, muulize taahira mwenzako Blater yuko wapi na uhuru wake wa FIFA.

Eti huru.
 
Yule msomali lazima akanyee debe lupango
 
Nimependa sana maneno ya Mwakyembe juu ya yule msomali wa Tff
Ni kweli TFF ni taasisi huru, ila ni mali ya serikali ya Tanzania. Huo uhuru unaousemea ni wa wapi?

Fifa pia walikua wakijidanganya wako huru, muulize taahira mwenzako Blater yuko wapi na uhuru wake wa FIFA.

Eti huru.
 
Lazima akanyee debe huyo msomali
huyo rais wa TFF Si ndio alisema atawashughulikia wanaoleta u Tundu lissu,,
Karma is Real.,,wakati wake sasa kutubu
 
Huyo Mwakyembe hana sauti tena katika soka la Tanzania hasa TFF.

Sio lazima uwe na Masters ili ujur kuwa Waziri wa Michezo ni nani katika nchi hii.

Sasa Mwakyembe hata Afcon hajaenda, lakini Waziri wa Michezo alienda kutia hamasa.
 
Tangu lini daktari wa mifupa akatibu Moyo?
Mwakyembe alitolewa ktk sheria na kupelekwa kwenye michezo
Which is which[emoji3]
 
Tunasubiri kwa hamu kuona huko kutunishiana msuli kutafikia wapi. Mimi hufarijika sana ninapoona watu wa si si emu wakiparuana.
 
Karia ni mmoja wa viongozi wa hovyo sijawahi kupata kuona huko Tifutifu toka enzi za kina Ndolanga na Mwanakatwe wanapokea fedha nyingi kutoka FIFA kila mwaka wao wapo busy na vikao tuu mbinu za kuendeleza soka Tanzania hakuna...Blatter ndie alikua mla rushwa mkubwa aliwadanganya Marais wengi kuwa wako huru na kutishia baadhi ya Nchi kuzifungia zikiingilia mambo ya soka mbona yeye mwenyewe alibanwa na hakuna lolote lililotokea na huyu Malinzi yupo ndani ingekua enzi za Blatter tungefungiwa hawa sasa hivi wanafanya kazi na Serikali sio vyama pekee...
 
Sawa karia
 
Alafu yule msomalia inaonekana anajeuri sana afu anashindana na wenzake et wako huru kivip ile s taasis ya serikali ama??
 
Ni kweli TFF ni taasisi huru, ila ni mali ya serikali ya Tanzania. Huo uhuru unaousemea ni wa wapi?

Fifa pia walikua wakijidanganya wako huru, muulize taahira mwenzako Blater yuko wapi na uhuru wake wa FIFA.

Eti huru.
Tena siyo ya serikali tuu Bali ya ccm na inatekeleza ilani ya ccm kama alivyo tangaza Makonda.
 

Mwakata kwenu, ngoja nikuambie kitu. Ili TFF ifanikiwe inahitaji ushirikiano mzuri baina ya waziri na wao. TFF haiwezi kufanya kazi bila waziri. Wanahitaji political buy in ili mambo fulani yaende. Wakiweka ukuta kati yao na waziri, mambo mengi yatawaendea kombo.
Walipaswa waende kwa waziri, wamsikilize. Baada ya hapo wangetoa sababu za kiufunzi za kwa nini wanafikiri Amunike apishe nafasi hiyo. Na sidhani kama waziri angeshupalia kocha amunike lazima abaki. Wangefikia tu muafaka mzuri. Tabia waliyofanya ni ya kitoto. Inapaswa wamuangukie waziri kwa kughafirika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…