Mwakilishi wa IMF asema, Tanzania haiwezi kuwa ya uchumi wa gesi

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
songosongo.jpg

TANZANIA haiwezi kuwa nchi ya uchumi wa gesi kama wengi wanavyotarajia bali rasilimali hiyo inaweza kuchochea sekta nyingine na kuifanya nchi hiyo kuwa ya uchumi wa kati, FikraPevu inaripoti.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Thomas...

Kwa habari zaidi, soma hapa => Mwakilishi wa IMF asema, Tanzania haiwezi kuwa ya uchumi wa gesi | Fikra Pevu
 
Bora washauri wanaotuamsha kutoka kwenye lindi la uzingizi, kuliko wataalam kama kina Muhongo wanaotulaghai mchana kweupe ...
 
Ni kweli kuwa ni vema kuchukua tahadhari. Wananchi wasiaminishwe kuwa kupatikana kwa gesi ndiyo suluhu ya umaskini wetu kwa muda mfupi. Wananchi lazima waelezwe na wanasiasa kuwa itachukua muda. Mpaka sasa huwa tunasikia malalamiko kutoka kwa wananchi wa Lindi na Mtwara, mathalani, wakihoji kuwa mbona hawana hiki au kile wakati mikoa yao inazalisha gesi?
 
Kama madini yote yanayochimbwa hayakusaidia nchi kuwa na uchumi wa kati, haiingii akilini kuamini gesi itatutoa kwenye umaskini, huo ndio ukweli aliousema huyo mtaalam.
 
kwani akiwa mwakilishi wa IMF ni nini ,gesi tunayomiliki ni nyingi mradi tu itumike vizuri yeye kafanya utafiti upi kwa hayo anayoyasema , gesi ndiyo inaendesha chumi kubwa kama russia na AAMERIKA yeye inakuwaje aibeze ikiwa Tanzania , tusidanganyane kila kitu ni usimamizi tu
 
Suala la msingi angesema namna gesi inavyoweza kuchochea uchumi kukua kwa kasi ya kutufikisha taifa la uchumi wa kati. Ni muhimu kuws macho na 'mabingwa' senye kubobea katika kushauri nchi zetu.

Kama ni wajuzi wa mambo kiasi hicho kwa nini nchi nyingi katika umoja wa ulaya zinayumba kiuchumi. Tukumbuke miaka ya 80 na 90 walikuwa na wimbo wa structural adjustment na ubinafishaji wa hola hadi nbc. Tuko wapi. Kwa kifupi kauli kama hizi za kutukatisha tamaa au kututoa kwenye mstari na mipango yetu madhubuti ipuuzwe.
 
Back
Top Bottom