Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 11,250
- 24,081
Ukiona serikali ya sisiyemu imetoka mbio mbio kutoa tahadhari ya janga la njaa na kuwasihi wakulima watunze chakula ujue hali si rafiki kabisa.
Mwigulu nchemba kageuka kuwa Yusuphu wa kwa farao kutabiri kuwa tutunze chakula maana hali si hali.
Japo yupo sahihi maana hali inajionyesha yenyewe kuwa mvua zimekuwa za mgao kama umeme wa Tanesco na mara nyingi hazipo kabisa.
Kwa wakulima wazoefu mtakubaliana na mimi kuwa huu ni wakati wa hasara kubwa sana kwa wakulima wengi.
Mazao mengi hasa mahindi karanga yameharibiwa sana na mvua.
Kwa upande mwingine kuna baadhi ya wakulima wachache wata neemeka sana.
Kuna baadhi ya maeneo kwao wanaema hali si mbaya sana.
Mfano maeneo ya biharamlo(kagera)
Chato geita na nyanda za juu kusini wao hali si mbaya kama huku kwetu shinyanga na baadhi ya maeneo ya Tabora,Geita,Dom,singida ,manyara nk.
Hawa kwa uchache wao watapiga hela sana pamoja na wafanyabiashara walio weka stoko nafaka zao.
Si mpunga si mahindi wala maharange watapa faida mara dufu.
Kwa watu wenye mpnago wa kuanza ufugaji huu ndo muda mzuri sana wa kununua mifugo kama mbuzi na ng'ombe.
Wafugaji huuza kwa bei yoyote Ile ili apate hela akanujue mahindi(chakula)
Hivyo baada ya tu ya sikukuu ya Xmass wewe Anza kununua mifugo yako ilishe vizuri kwa miezi4 mbele then utakuja hapa na sadaka yako.
Ni rahisi sana kununua mbuzi kwa 70k then ukaja ukauza 200k! Baada ya miezi hiyo 4 au zaidi.
Kilimo kingine ambacho kitatupa faida wakulima hasa wenye mitaji ya kati na mikubwa ni kilimo cha umwagiliaji.
Zingatia kwenye ukame au uchache wa mvua vyanzo vingi vya maji hukauka hivyo ili utoboe walau uwe na water pump machine ukubwa wowote ule Inch2,3au 4 zote ni sawa tu.
Ukumbuke hata kenya hali si hali uganda wao si mbaya kivile japo siku zote ni wategemezi wetu hao wote akiwemo na mjomba kagame.
Kule Malawi,msumbiji mimi sina ufahamu sana kama na wao wanategemea sana bidhaa za kilimo kutoka kwetu.
Zaidi ya yote na wapa pole kwa hasara kubwa tulizopata msimu huu lawama zote ipewe ccm na machawa wake wote.