Nani kasema hatumtaki Rage agombee kwani kabla yake si alikuwepo Hayati Juma Kaboyonga ambapo Rage alishinda kura za maoni??
Ndugu yangu CCM ina utaratibu wake mnaweza mkachukua Fomu watu 100 lakini mshindi atakuwa ni mmoja tu kwenye Kura za maoni.
Shauri yake agombee au asigombee lakini Demokrasia katika mchakatoi wa Kura za maoni itafanya kazi.
Hapa ndipo ninapoikubali CCM kupitia hatua za uteuzi.
Nakuonea huruma kwania Tabora Mjini itaendelea kuongozwa na Wabunge kutoka CCM!
Huh! Hivi ndivyo magamba mnavyojidanganya eeh?
Majigambo yako hayana tofauti na yule Waziri wa Habari wa Sadam Hussein (R.I.P), ambayo yalitoweka ghafla baada ya Iraq yote kuvamiwa na majeshi ya USA!
Are you serious Mkuu? Ama unajifurahisha tu?
Mimi pamoja na chama changu, nakuhakikishieni kuleta mabadiliko hayo.
CDM ni kama kimbunga ama mafuriko, mpende msipende mtasombwa tu!