Mwadui FC ipo tayari kumpokea Paul Nonga akitaka kurudi

kategile

Member
Dec 25, 2014
18
1
050663c5a2736a8f01d94819fc1a46c1.jpg
STRAIKA wa Yanga, Paul Nonga amekuwa
akikumbana na ushindani mkubwa ndani ya
kikosi hicho kutoka kwa mastraika wa kigeni,
Amissi Tambwe na Donald Ngoma lakini
uongozi wake wa zamani wa Mwadui FC
wamemfungulia milango kama atahitaji
kurudi kwao.
Yanga ilimsajili Nonga akitokea Mwadui FC
kwa mkataba wa miaka miwili lakini
anashindwa kupata nafasi ya kucheza mara
kwa mara ili kuonyesha cheche zake ndani
ya kikosi hicho kinachoshiriki michuano ya
kimataifa ya Mabingwa wa Afrika.
Kulikuwepo na taarifa kwamba huenda Yanga
msimu ujao wa Ligi Kuu wakamrudisha
kwenye timu yake ya zamani kwa mkopo
ikiwa ni lengo la kumsaidia kupata nafasi ya
kucheza mara kwa mara ambapo Katibu
Mkuu wa Mwadui FC, Ramadhan Kilao
amesema milango kwa Nonga iko wazi.
"Hata alipokuwa anaondoka tulimwambia
akijisikia kurudi kwetu ni ruksa. Nonga bado
ni mchezaji mzuri ila tatizo lipo kwenye
ushindani wa namba.
"Kuna wachezaji wa kulipwa pale ambao si
rahisi kuwakalisha benchi, hivyo kama
itatokea Yanga wakaamua kumrudisha kwetu
kwa mkopo sisi hatuna tatizo tutamkaribisha
na kumpokea," alisema Kilao
Mwadui kwa sasa inajiandaa na mechi dhidi
ya Yanga huku ikisubiri kupangiwa timu
pinzani kwenye michuano ya Kombe la FA
katika hatua ya nusu fainali ambapo timu
tatu tayari zimetinga hatua hiyo ikiwemo
Yanga na Azam.
Timu ya Simba na Coastal Union zinasubiri
kucheza hatua ya robo fainali ili apatikane
mshindi atakayetinga hatua ya nusu fainali
kuungana na timu hizo.
 
Back
Top Bottom