Mvumilivu hula mbivu

Mvumilivu hula mbivu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,863
"Jambo kubwa duniani miongoni mwa mambo yanayowaangusha wengi ni KUKOSA UVUMILIVU, naam kukosa uvumilivu imekuwa ni chanzo cha watu wengi kuangamia kwenye maeneo mbalimbali ya maisha."

"iko ivi miongoni mwa sababu zinazofanya watu wengi kukosa uvumilivu ni kutaka mafanikio ya haraka, na kingine ni kuzikimbia changamoto wanazokumbana nazo kwenye eneo wanalotaka waone mafanikio, hivyo hali hizo mbili huwafanya baadhi ya watu washindwe kuvumilia pale wanapopita kwenye wakati mgumu."

"Tambua ya kuwa ukikosa UVUMILIVU kwenye ulimwengu huu daima utakuwa ni mtu wa kunung'unika tu, yaani maisha yako yatajawa na lawama tele kwa kila jambo linatokea maisha mwako."

"Yawezekana nawe kuna jambo unalitazamia lifanikiwe kwa muda mrefu, na hali hiyo imekufanya uhisi kufika mwisho wa kuvumilia, nakusihi usichoke kuvumilia ndugu yangu maana kila watu unaowaona wamefanikiwa kwenye maisha tambua ya kuwa walivumilia magumu mengi sana, hivyo subira yao imewafanya wafike hapo walipo leo."

"Ni kweli unataka mafanikio ila cha kushangaza ni kwamba hautaki kuwa mvumilivu, tambua ya kuwa usipokuwa mvumilivu ni rahisi kuyapiga teke MAONO yako na ukakumbatia ya wengine, na mwisho wa siku ukaendelea kuwa mtumwa kwenye kila eneo la maisha yako."

MFANO HALISI:-

"Je umewahi kuona wapi ukapanda mahindi leo na ukavuna kesho?, na imani hujawai kuona jambo hilo hata siku moja, maana mahindi yana kipindi chake cha kuvunwa baada ya kupandwa yaani zipo mbegu ukulazimu kukaa ukisubiri kwa muda wa siku 90 ndipo ukavune mahindi yako, hivyo basi kama utakosa uvumilivu wa kusubiri na ukalazimisha upande mahindi leo na kesho ukavuna tambua hakuna utakachoambulia zaidi ya kupata mbegu hizo-hizo."

"Ndivyo ilivyo kwenye maisha, nikianza na hatua za ukuaji wetu sisi wanadamu, iko hivi hauwezi ukazaliwa leo alafu kesho yake ukatembea, ni lazima upitie hatua za ukuaji yaani uwe mtoto, alafu uwe kijana, na ndipo uwe mzee, maana yake ni kwamba hauwezi ukaanza kuwa mzee ndipo ukawa kijana, yote hayo yanahitaji uvumilivu, lakini pia hata kwenye shughuri za kila siku za maisha uvumilivu ni wa lazima sana."

"Kwa maana kila maono yana muda wake wakutimia, hivyo basi huwezi ukaanza biashara leo kwa mtaji wa elfu 50 alafu kesho uwe na mtaji wa milioni 1, kwa hiyo unahitajika uvumilivu wa kutosha huku ukiendelea kufanya biashara na baada ya muda kupita ndipo utaanza kuyaona mafanikio na mtaji wako ukikua, sasa kama utalazimisha mtaji wako ukue haraka nje ya muda halisi basi jiandae kupotea kwenye biashara."

"MVUMILIVU HULA MBIVU maana yake ni kwamba nguvu ya kuvumilia changamoto chanya unazokumbana nazo kwenye eneo ulilopo inaweza kukufanya ukayapokea mafanikio kwenye jambo ufanyalo."

"Katu usidanganywe na hadithi za vijiweni kwamba utalala maskini na uamke tajiri, pole! kila jambo linahitaji UVUMILIVU maana ukikosa uvumilivu ni rahisi kukata tamaa."

"Ni magumu mangapi yamekupata kwenye safari yako ya maisha, je upo tayari kuyaruhusu magumu hayo yaue MAONO yako makubwa uliyonayo?, yaani magumu yakutengenezee mtazamo hasi kuhusu maisha?, haya ndio madhara ya kukosa uvumilivu, kukata tamaa, kuwa na mtazamo hasi kuhusu maisha, kujiua, na mengine mengi yanayotokana na kukosa uvumilivu, kwa hiyo kama hauko tayari basi nakusihi usichoke kuvumilia.ndugu yangu."

"Ni kipi umepitia au unapitia kwa sasa?, hivyo nakusihi daima usichoke kuvumilia, kwa hiyo zidi kumtegemea Mungu na ufanye kazi kwa bidii huku ujifunza kila siku, na kama ni kwenye mahusiano umeumizwa basi tulia na msihi Mungu akusaidie."

"SUBIRA YAVUTA HERI"
 
sio yote ya kuvumilia, baadhi watakiwa ongea na kupigania haki yakoo

Eti uko na girl/boy friend wako yeye anachepuka hata hamjafikia ndoa ..... vumilia ukitegemea atakuja kuwa mtulivuuu mwishi kwa amanii..we vumilia tuuu.....mbutanangaaaaa
 
Back
Top Bottom