Mvua za Masika kusababisha Mafuriko

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za masika katika ukanda wa Pwani, zinazotarajiwa kuanza wiki hii, zitakuwepo kwa vipindi vifupi na zitakuwa kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko. Aidha, kwa wakati huo hali ya joto kali itaendelea kuwepo nyakati za usiku huku ikipungua nyakati za mchana.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi alisema hayo jana wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kueleza kuwa mvua za masika zimeanza kama ilivyotabiriwa huku ukanda wa Pwani zikianza wiki ya kwanza ya mwezi Aprili.

Dk Kijazi alisema ingawa maeneo hayo ikiwemo Jiji la Dar es Salaam, yanaonesha kuwepo mvua za wastani hadi chini ya wastani, lakini mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa.

“Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa wakati wa msimu huo wa masika na kuweza kusababisha hata mafuriko, ni vema wananchi kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa vipindi vifupi,” alisema Dk Kijazi.

Alisema hali ya joto wakati huo wa mvua, inaonesha katika utabiri kupungua nyakati za mchana wenye kiwango cha juu cha joto huku usiku likiendelea kuwa kali kama ilivyo sasa licha ya kuwa kiwango chake ni cha chini.


Chanzo: Habari leo
 
Dar ndio tz, sasa na sisi wakulima tulioandaa mashamba anatoa ushaur gani?

Kama ni mkulima pole sana.Growing season kwa ukanda wa pwani itakuwa fupi sana,only about forty five days.Hii haitatosha even for short duration maize varieties,mtama au hata mihogo hasa ukizingatia the high evapotranspiration rates zilizopo sasa kwa sababu ya joto kali.Ardhi inakauka haraka sana.Serikali ijiandae kuwapatie wananchi chakula cha msaada.Hali sio nzuri hata kidogo.
 
Back
Top Bottom