Mvua katika jiji la Dar es Salaam

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba sasa mvua inanyesha katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Mvua ina baraka na matatizo yake. Moja ya tatizo la mvua ni mafuriko kama yalivyoripotiwa sehemu mbalimbali za nchi yetu ikiwemo Kilosa mkoani Morogoro. Watu wengi wamepoteza mali zao na wengine wamepoteza maisha yao.


Mvua inayonyesha katika jiji la Dar es Salaam imeleta matatizo kadhaa kama vile maji kufurika maeneo mbalimbali ya jiji na ongezeko la mazalia ya mbu. Katika maeneo ya Manzese imekuwa ni kero kwa wapenda mazingira safi na imekuwa ni neema kwa wenye vyoo kwani wametumia mvua hiyo kuzibua vyoo vyao. Baada ya muda kidogo kupita ninadhani tutaanza kusikia milipuko ya magonjwa kama kuhara, kipindupindu na mengineyo. Nini kifanyike ili kunusuru afya za raia wema. Wakati mwingine ni ngumu kutoa taarifa polisi kwani uzibuaji wa vyoo hufanyika usiku wakati watu wengi wamelala.
 
Back
Top Bottom