Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,174
- 10,650
Mbeya. Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari unatarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa marekebisho.
Nape aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wadau wa habari, utamaduni, wasanii na michezo kutoka mikoa ya Mbeya na Songwe jijini hapa.
Awali, muswada huo uliondolewa bungeni mwaka jana baada ya kupigiwa kelele na wadau kwa madai kuwa ulikuwa ukihitaji kufanyiwa marekebisho katika baadhi ya vifungu.
Hata hivyo, Nape alisema jana kuwa tayari marekebisho yameshafanyika na sasa upo kwenye hatua ya mwisho kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni.
Alisema muswada huo umebeba mambo mengi yanayohusu maslahi ya waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na masilahi mbalimbalimbali ya waandishi, likiwamo suala la mikataba ya kazi, bima ya afya na mazingira ya mazuri na rafiki ya kufanyia kazi.
Nape alizungumzia suala la utitiri wa vyuo alivyodai kuwa vingi havina sifa ya kutoa taaluma ya uandishi wa habari na kusema kuwa vitaondolewa kupitia sheria itakayotokana na muswada huo.
Alisema lengo ni kutaka krudisha heshima ya tasnia pamoja na kujenga heshima ya kazi hiyo kwa kuzingatia weledi.
Awali, akisoma taarifa, Katibu Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (MBPC), Emmanuel Lengwa alisema kuna changomoto zinazowakabili waandishi wa mikoa ya pembezoni ikiwa ni pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi na wengi wao hutumikishwa kwa muda mrefu bila kuwa na mikataba ya ajira na wengine bila malipo. “Lipo tatizo kubwa la kuporomoka kwa maadili na misingi ya taaluma ya habari nchini, pia tunatambua kuwa wewe ndiye mwenye dhamana ya kusimamia ubora na maadili ya wanahabari,” alisema Lengwa.
Alisema Serikali ina uwezo wa kutunga sheria bora itakayowakomboa waandishi nchini kuliko hii ya sasa.