Muswada wa fedha: Kamati ya bajeti imebariki wananchi kubebeswa mzigo mkubwa kodi

masalia

Member
Dec 20, 2012
24
26
Katika taarifa iliyosomwa na Mh. Ntemi Chenge (MB) (Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti) pamoja na mambo mengine amesema waliowasilisha majedwali ya mabadiliko kwenye sheria ya fedha walishindwa kutoa vyanzo mbadala vya mapato ya Serikali. Sio kweli kwamba wote waliofanya hivyo hawakuwasilishwa vyanzo mbadala.

Naambatanisha Jedwali la Mabadiliko lililowasilishwa Bungeni na Mh John Mnyika (MB) kwa madhumuni ya kuondoa kodi zinazowakandamiza wananchi na kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha.

Ntaelezea kwa kifupi mazumuni ya mabadiliko aliyoyalenga.

Kwanza kuondoa tozo inayopendekezwa kuwekwa na Serikali kwenye huduma za ''voice menu'' na ''call blocking''
_ katika hili Mnyika anasema voice menu inatumiwa na watumiaji wa simu mahalumu (walemavu) (wasiiona) na hivyo kuwatoza kodi wakati wanatumia menu za kawaida kwenye simu zao hawatozwi ushuru si sahihi kisheria kwani tozo hiyo ni ya kibaguzi.
_kuhusu call blocking ni huduma inayolenga kulinda faragha ya mawasiliano, yaani mtu asipota kupigiwa simu na mtu fulani, basi ana'block na hilo ni swala la privacy ya mawasiliano hivyo pia si hahihi kutoza ushuru huo.

Pili Mnyika analenga kupunguza tozo inayopendekezwa na serikali kukata wananchi kiasi cha shilingi 0.15 kwa kila muhamala wa pesa kwa njia ya simu (M-Pesa, Airtel-Money, Tigo Pesa, Zantel n.k) kwa kila muhamala wa kuanzia shilingi 30,000/-
_katika hili Mnyika anapendekeza makato yawe shilingi 0.1 kwa watumaji na wapoleaji pesa zinazozidi shilingi 50,000/- lengo likiwa ni kulinda wananchi masikini wasilipe kodi nyingi kwa huduma wanayoitegema ya mobile money.

Zaidi anapendekeza kuondolewa kwa tozo za mafuta ya taa, disel, petroli na mafuta mengine yote ili kumuondolea mziogo wa kodi mwananchi, kuthibiti kupanda kwa nauli, kupunguza gharama za usafirishaji, na kuthibi kupanda kwa bei ya chakula na hivyo kuthibiti mfumuko wa bei, (inflation).

Zaidi anapendkeza makampuni ya simu yalipe kodi kwa mapato wanayoyapata kupitia mobile money transfer.
Kuwapunguzi msamaha wa kodi wawekezaji.

Nimeambatanisha Jedwalia la Mabadiliko la Mnyika, na Vyanzo vipya vya mapato alivyovipendekeza na kamati ya Chenge ikakataa.
 

Attachments

  • mbadala.pdf
    190 KB · Views: 172
  • jedwali.pdf
    60.1 KB · Views: 97
Chenge ni mwanasheria uchwara anayetumia siasa kujificha na anajua kurubuni watu sana na CCM wanamkubali kwa ufisadi wake
 
Nimesoma mapendekezo ya Mnyika naona yapo very shallow.

Watanzania tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa, hii bajeti yetu tegemezi kwa 30%, wengi wetu hatulipi kodi.
 
Nimesoma mapendekezo ya Mnyika naona yapo very shallow.

Watanzania tulipe kodi kwa maendeleo ya taifa, hii bajeti yetu tegemezi kwa 30%, wengi wetu hatulipi kodi.

Wananchi wengi hawalipi kodi sio kwasababu hawapendi ila kwasababu kodi zao haziwaletei maendeleo badala yake zinatumika kwa kusafiria viongozi na kununua mashangingi pamoja na kufanya seminar kule Ngurudoto. Kodi zao zingekuwa zinatumika vizuri na wao kuridhika kuwa zinawaletea maendeleo wasingekuwa na kigugumizi kulipa kodi!!!
 
Back
Top Bottom