Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,247
- 25,191
Akizungumza katika semina kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini, Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Sarah Maongezi, alisema kuna uwezekano muswada huo ukawasilishwa katika mkutano ujao wa Bunge wa Septemba.
Semina ya wahariri ilihusu utekelezaji wa Mkataba wa Kudhibiti Tumbaku wa Shirika la Afya Duniani (WHO FCTC) na ilifanyika juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Maongezi ambaye pia ni Mratibu wa Saratani wa wizara hiyo, alisema tumbaku inasababisha vifo vya watu zaidi ya milioni sita kila mwaka na wengi wao wapo kwenye umri wa kuanzia miaka 30 hadi 69 ambao bado wana uwezo wa kulitumikia taifa.
"Serikali ina dhamira ya dhati ya kudhibiti tumbaku. Kuna uwezekano muswada wa kuidhibiti ukawasilishwa bungeni katika Bunge la Septemba," alisema.
Aliongeza: "Tumbaku ni bidhaa pekee ambayo imehalalishwa kutumika, lakini inaua karibia nusu ya watumiaji kama itatumika kama ilivyokusudiwa na wanaoitengeneza.
"Katika karne hii ya 21, watu milioni 200 ni wahanga (waathirika) wa matumizi ya tumbaku, na ndiyo karne ambayo inakadiriwa kuua mabilioni ya watu, kama mwenendo hautabadilika."
Alisema asilimia 14.1 ya Watanzania sasa wanavuta tumbaku kila siku wakati kileo hicho ni kisababishi kikuu cha magonjwa makuu yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa ya mfumo wa hewa na kisukari.
Alisema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanasababisha asilimia 60 (milioni 35) ya vifo vyote duniani, ambapo vifo karibia asilimia 80 (vifo milioni 28) hutokea kwenye nchi zilizo na kipato cha chini na cha kati.
Makadirio ya WHO ya mwaka 2010 yanaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia asilimia 27 ya vifo vyote vinavyotokea nchini.
Dk. Maongezi alisema mwaka 2008 ilikadiriwa kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yalisababisha vifo 75.7 na 58.8 kati ya watu 1,000, na asilimia 42.8 wanaume na asilimia 28.5 wanawake walikuwa chini ya umri wa miaka (60).
"Kwa bahati nzuri tunafahamu njia za kuchukua ili kupambana na janga la matumizi ya tumbaku na kuthibitisha utabiri huo usiofaa kuwa siyo sahihi," alisema.
"Hatua zote hizo zipo mfumo wa WHO FCTC. Mkataba huu uliridhiwa mwaka 2005 na hadi hivi leo una washiriki 180, ambao wanawakilisha karibia asilimia 90 ya idadi ya watu duniani. Tanzania iliridhia mfumo wa mkataba wa kudhibiti matumizi ya tumbaku Aprili, 2007.
"Shirika la afya duniani limezungumzia mkataba huu kuwa ni chombo kizuri kitakachoweza kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mnamo mwaka 2011, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Margreth Chana, kwenye kilele cha mkutano wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, alisema tukitekeleza kwa asilimia kubwa mkataba huu, tuna uwezo wa kuyapiga magonjwa ya moyo, saratani, kisukari, na magonjwa ya mfumo wa hewa."
Alisema utekelezaji wa WHO FCTC umejumuishwa kwenye Malengo Endelevu ya Milenia Namba Tatu, hivyo kuandaliwa kwa muswada huo kutakuwa na utekelezaji wa udhibiti wa tumbaku.
Alisema miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuwamo kwenye muswada huo ni kudhibiti uvutaji holela wa sigara na kupambana na mbinu chafu za matangazo ya tumbaku hasa kwa watoto.
Dk. Maongezi ambaye amefanya kazi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa zaidi ya miaka 10, alilipongeza Shirika la Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku (TTCF) kwa kubuni mkakati huu wa kuwajengea wahariri uwezo wa kuandika makala za tumbaku kwa umahiri huku wakiwa na takwimu za uhakika na kuushukuru Mtandao wa Kiafrika wa Kudhibiti Tumbaku (ATCA) kwa ufadhili uliowezesha semina hiyo ya siku mbili.
KILA SEKUNDE 8
Katika semina hiyo, mwakilishi wa ATCA, Deowan Mohee, alisema tumbaku ni hatari ikitumika kwa vyovyote.
Alisema tumbaku ina kemikali zaidi ya 4,000 zikiwamo za sumu kama vile nikotini, lami (tar), kaboni monoksidi, arsenic na benzopyrene na kwamba madhara yake yanajumuisha kuua kidogo kidogo viungo vya mwanadamu na nyama (tissues).
Akinukuu ripoti za WHO ya mwaka 2010 kuhusu tumbaku, Mohee alisema kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki dunia ulimwenguni kutokana na matumizi ya tumbaku. Alisema inaaminika pia kwamba watu saba kati ya wavutaji tumbaku 10, huanza matumizi hayo wakiwa watoto.
Ripoti za shirika hilo zinasema kadri mtu anavyoendelea kuvuta tumbaku kwa muda mrefu, hufupisha urefu wa maisha yake kwa takribani miaka 20 hadi 25 kutokana na kuingiza mwilini kemikali hizo zaidi ya 4,000.
Alisema uchunguzi umebaini zaidi ya asilimia 80 ya chembe za moshi unaovutwa kwenye sigara hubakia mwilini na kwamba wataalamu wameonya kuwa ikiwa mambo hayatobadilika, kufikia mwaka 2030, uvutaji wa sigara utasababisha vifo vya watu zaidi ya milioni nane kila mwaka.
Alisema athari za tumbaku zinaanzia kwa mkulima wa zao hilo, familia yake na hatimaye mvutaji na watu wanaokaa karibu na wavutaji nao.
Aliongeza kuwa upo ushahidi wa kutosha wa kisayansi kwamba moshi wa sigara usiokuwa wa moja kwa moja, husababisha magonjwa sawa kama sigara inayovutwa moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo na mishipa, mapafu na upumuaji (COPD).
Kutokana na hali hiyo, maelfu ya watu wasiovuta sigara nao hufariki dunia kila mwaka kutokana na kuishi au kukaa karibu na watumiaji wa tumbaku.
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Baraza la Taifa la Kupambana na Uvutaji Sigara Afrika Kusini, Yussuf Saloojee, alisema kuwa kila dola moja inayotumika kununua sigara inasababisha hasara ya dola sita.
Alisema Afrika Kusini imefanikiwa kupunguza matumizi ya tumbaku kutokana na mbinu mbalimbali zikiwamo za kutunga sheria kali dhidi ya matangazo na utumiaji wa tumbaku na kuongeza kodi kwenye sigara.
Naye Mwakilishi wa WHO-Tanzania, Dk. Neema Kileo, alisema kuwa mbali na kusababisha umaskini kwa wakulima wake, tumbaku ina athari hasi kwa jamii na uchumi wa nchi kutokana na kuharibu mazingira, utumikishwaji wa watoto unaowapelekea kukosa masomo na taifa kupoteza nguvu kazi kutokana na vifo vya watumiaji wake wengi.
Chanzo: Nipashe