Kalamu Huru
Member
- Dec 2, 2017
- 11
- 8
Salamu..!!
Kwa muda mrefu nimefuatilia kwa mbali mwenendo wa siasa nchini mwetu. Nimesikia na hata kushuhudia Chama Tawala CCM kinavyofanya kila namna kuufifisha upinzani nchini. Na nimesikia namna upinzani unavyolalamikia jambo hili.
Siku za karibuni umefanyika Uchaguzi katika kata 43 na sote tunajua kilichotokea. 42 - 1. Sababu za kushinda kwa CCM zinaeleweka na zile za kushindwa kwa Upinzani zinaeleweka.
Nimejiuliza, je, sababu zitolewazo na Upinzani juu ya kushindwa kwao, zinatosheleza? Zina mantiki kwa uendelevu wa upinzani nchini? Je, kuna siku sababu hizi zitabadilika?
Ni muhimu kuelewa kuwa, siasa za chama tawala dhidi ya Upinzani ni kama mchezo wa hide and seek. Upande mmoja unajitahidi sana kufichama na mwingine unajitahidi sana kumtafuta aliyejificha na kumfichua. Anayefanikiwa katika kujificha au kufichua ndio huwa mshindi.
Hivyo, kwa mfano huo, ni wazi kuwa, chama tawala kitatafuta na kutumia mbinu mbalimbali ili kuweza kuufifisha Upinzani, na Upinzani unapaswa kubuni mbinu mpya bora zaidi kila wakati ili ubaki pasi kufifishwa na zenye kuweza kufanya kazi na kupelekea ushindi katika mazingira yaliyopo. Kulalamika kuwa mazingira ya kisiasa yamebinywa n.k ni sawa kabisa na kukiri kuwa upinzani umeishiwa ubunifu wa mbinu mbadala zenye kuweza kufanya kazi katika mazingira haya halisi tuliyomo.
Utetezi huu, ukiutafakari kwa kina, ni wa kukata tamaa. Hauna afya kwa siasa za Upinzani nchini.
Ni muhimu sana kwa Upinzani wetu kujipanga upya, na kubuni mbinu bora mbadala za kuuwezesha kutofifishwa na kubaki kutumainiwa na wafuasi wake na kuufanya upinzani kuwa endelevu nchini.
Wasalaam....!
The Quill.