mussa banzi aliharibu mambo baada yakuanza kuigiza kama leading star kwenye movie zake, wakati hajui kuigiza... wakali wenye mvuto na ujuzi wakuigiza leading roles akawa anawabania, hence kushuka kwako kwenye soko.
ryt now yupo yupo anafaidi mauzo ya movie zake za zamani huko africa magic na zuku.. but coming back with a hit??? sijui
Yap mkuu hata Mimi nilimuona kwenye movies kadhaa, wengi hawakupenda uigizaji wake , japokuwa ni muongozaji na mtunzi mzuri sana kwangu Mimi, Jamaa anajua na ni bonge la mbunifu alinifuraisha sana kwenye movie ya VERONICA
Tamba ni mtunzi mzuri sana wa hadithi ...kama hadithi zake zingepata waongozaji wazuri na kuwekwa kwenye sinema nafikiri zingekuwa nzuri sana...huyo Banzi pia sio mbaya ana sinema flani za asili asili (sijui ndie mwenyewe au namchanganya)...ila technolojia yetu ipo chini sana kiasi kwamba hadithi nzuri zinashindwa kuwekwa kwenye sinema na kueleweka.
Kweli Mussa Banzi alikuwa mtunzi mzuri na hata michezo ya Kaole enzi zile ITV alikuwa anawatungia akishirikianana Chrisant Mhenga mf igizo la Radi.
Ila baada ya kuanza kujipa promo mwenyewe ihali hajui kaharibu kila kitu bora tu arudi fani yakeileile maana story zake zilikuwa nzuri.
Binamu umenikumbusha hizo movie karibu robo tatu ya ulizotaja home zipo hapa Tena ni za VHS lol! Nikiziangaliaga nacheka sana.
Yes binamu kumbe unamjua aliwahi kushiriki pia kwenye utunzi kaole miaka hyoo, Jamaa anajua sana ila kuigiza ki ukweli akaoge, napenda sana movie yake ya SIKIO LA KUFA na FUNGU LA KUKOSA dah Jamaa anajua nilimkubali zaidi kwenye VERONICA aliyocheza odama dah ni noma sana , halaf kuna wale wazee anapenda kuwatumia Sijui mzee msisiri na yule bi chonde , dah couple yao ya ukweli sana
Teh teh umenikumbusha gwiji lao bi Chonde yule mmama ana act utadhani ni kweli sio maigizo.
Yah yuko poa sana, anaigiza vizur cha ajabu ma producer hawamchukuagi yaani movie za mussa banz tu ndo yupo sana, huyu Odama nae cjui kwa nn hawap shavu hawa wazee maana ndo walikuwa wanaigizag kama wazazi wake na walikuwa wanapatia hatari, siku izi cjui yuko wapi , ila msisiri namuona kwenye movies nyingi tu
Ndiyo yeyeTamba si alitunga ile movie maarufu ya girlfriend?..