Hakuna wa kumfikia Kibwana Mwinyimkuu (Chili Sosi ) 'scenes' za uganga

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,361
21,051
Hakika mwigizaji Jumanne Rajabu mwanzoni alikuwa anafahamika sana kwa jina la uchekeshaji la Chili Sosi au Chili akiwa na swahiba wake Ringo baada ya kuamua kuuvaa uhusika wa mganga wa kienyeji hakamatiki hata kidogo.

Chili ameigiza filamu nyingi sana za uchekeshaji ila filamu zilizompa umaarufu zaidi ni zile alizocheza kama mganga wa kienyeji.

Chili alianza kuonesha utofauti wa kuuvaa uhusika kutoka uchekeshaji mpaka scene za u serious kupitia filamu ya Tabana iliyoongozwa na Sultani Tamba.

Katika hiyo filamu ya Tabana ,mama yake mzazi wa Chili alikuwa gwiji wa wachawi hapo kijijini na alikuwa katika hatua za mwanzoni za kumrithisha uchawi Chili.

Mbali na filamu ya Tabana,Chili alionesha uwezo mkubwa sana kupitia filamu ya Shumileta (Queen of the devil) akiwa ndiye mganga pekee aliyeweza kumdhibiti vilivyo Shumileta na kumfungia kwenye kopo kisha hilo kopo kumkabidhi mteja wake Monte (Odama)aende kulifukia chini ya ardhi.

Chili pia alionesha makali ya hali ya juu sana kupitia filamu ya Kihongwe nguvu za giza iliyotungwa na Mussa Banzi.

Mbali na Kihongwe, Chili alionesha uwezo mkubwa kwenye filamu ya Chite Ukae (neno la kizaramo lenye maana ya rudi nyumbani).Muigizaji mkuu katika hiyo filamu ni Rehema Msangule au ukipenda muite Dorlin ambaye alicheza pia filamu ya Insyuka.

Kwenye filamu ya Chite Ukae,njia pekee ya kutibu matatizo ya Dorlin ilikuwa ni kurudi nyumbani (kufa) sasa je nini kifanyike ili aside na ili asiendelee kusumbuliwa na wachawi, majibu kamili aliyatoa muigizaji Chili Sosi.

Mbali na filamu ,Chili Sosi ameendeleza ubabe pia mpaka kwenye tamthiliya na huku amezidi kujizolea umaarufu na mashabiki kwa kiasi kikubwa mno na mpaka jina likabadilika kabisa kutoka Chili mpaka Kibwana Mwinyi Mkuu.

Kwa hapa Tanzania sioni msanii yeyote atakayeweza kumpiku Chili Sosi (Mwinyi Mkuu)katika kuuvaa uhusika was uganga wa kienyeji.

Screenshot_20210715-022815_1626307109611.jpg
 
Nilimkubali uyu jamaa kwenye hile tamthilia waliocheza na kitale, jina limenitoka kidogoo
 
Yaan ile tekelo mmamaaa ee wamkoma tekelo mmamaa! Yaan kwenye hii tamthilia mwinyi mkuu na mtawala waliuvaa vizuri uhusika! Kuna nyingine huyu mtawala amecheza tofaut namaneno yakuambiwa?

Mtawala ,tofauti na maneno ya kuambiwa labda kuna tamthiliya ya binadamu huenda akawepo maana waigizaji walioigiza maneno ya kuambiwa ndio hao hao watakaoigiza tamthiliya ya binadamu.
 
Nlimkubali sana kweny shumileta prt 2
Aliifanya iwe Bora kwa movie zote
Za kutisha kibongo bongo
 
Back
Top Bottom