Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba wanasayansi nchini humo wamepiga hatua kubwa sana katika kupata tiba dhidi ya Corona.
Katika hotuba kwa taifa jana jumapili, Museveni amesema kwamba wanasayansi nchini humo wamefanyia majaribio tiba hiyo ambayo hakutoa maelezo zaidi, akiongezea kwamba kwa sasa, madaktari wanatumia mchanganyiko wa vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini dhidi ya virusi vya Corona.
โwanasayansi wetu wameniambia habari njema kwamba wameunda dawa saba tofauti. Sita kati ya hizo zinafanyiwa majaribio na moja inaongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.โ Amesema Museveni katika hotuba iliyopeperushwa na runinga zote za habari nchini Uganda, akiongezea kwamba โdawa za kwanza tatu zinauwa virusi hivyo na kuzuia uharibifu mwilni.โ
Museveni amesema kwamba dawa hiyo imefanyiwa โmajaribio kwa wagonjwa kadhaa wa Corona na kupona na itaanza kutumika vikamilifu kwa watu wote Desemba tarehe 15 mwaka huu.โ
Ameendela kusema kwamba โkatika mda wa siku 40, dawa hiyo itakuwa imetibu watu wengi na kuweka Imani kati yaw engine kwamba inaweza kutibu Corona na virusi vingine.โ
Museveni ameongezea kusema kwamba โwanasayansi wa Uganda wamezindua vipimo vya Corona kwa kuumia sampuli ya mate na kutoa matokeo ndani yam da wa dakika 30.โ
Jumla ya watu 210 wamefariki kutokana virusi vya Corona nchini Uganda.
Kampuni kadhaa nchini Marekani na ulaya zimetangaza kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona.