"Muogope kama ukoma" vs "Aatapata nje ya CCM"

"Muogope kama ukoma" vs "Aatapata nje ya CCM"

Ntullinze

Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
37
Reaction score
8
Kamwe mtu huwezi kutengeneza historia endapo tu huijui historia, bali ni wale tu wanaoijua historia ndio pekee wanaoweza kutengeneza historia.

Mnamo mwaka 1967, baadhi ya mataifa ya nchi za kiarabu chini ya uongozi wa kiongozi wa taifa la Misri (Abdul Nasser), yalianzisha mkakati wakutaka kulifutilia mbali taifa la Israeli. Lakini baada ya mapigano ya takribani siku sita, Abdul Nasser siyo tu kwamba alipoteza ndoto yake hiyo bali jeshi lake pia liliangamia na zaidi ya yote Abdul Nasser alipoteza hadhi yake pia! Baada ya miaka mitatu Abdul Nasser alikufa kwa mshituko wa moyo; rafiki zake walisema amekufa kwa sababu ya kukata tamaa. Lakini kitu ambacho kilifurahisha zaidi katika harakati hizo ni pale tu ambapo hata wale ambao walikuwa ni maadui wakubwa wa Abdul Nasser walimuunga mkono Abdul Nasserakiwemo mfalme Hussein wa Saudi Arabia!

Hapa nchini Tanzania, hivi sasa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 ambapo wananchi tutakuwa na fursa na pia uwezo wa kuchagua madiwani, wabunge pamoja na mtu yule ambaye atakuwa ni raisi wa awamu ya tano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na katika mchakato huu, tumekuwa tukishuhudia na tutazidi kushudia mambo mengi sana na hasa hasa kuhusiana na ama vyama vyetu vya siasa au wana siasa wetu.
Katika harakati hizi, tumeshudua wanasiasa wakihama kutoka chama hiki na kwenda kile, tumeshuhudia kauli nyingi mpaka sasa ikiwemo "kakatwa" ama "kukatwa" n.k

Binafsi mimi napata kigugumizi kidogo kujua kama hii ndiyo kukua kwa demokrasia ama ni uchanga wa demokrasia au ni kuongezeka kwa uelewa ama uchanga na ufinyu wa kufikiri! Hivi, ili mtanzannia uweze kuwatumikia wananchi ama taifa lako ni lazima uwe diwani?, ni lazima uwe mbunge? ama ni lazima uwe raisi? ndip ujitanabaishe kwamba wewe ni mzalendo na una uchungu sana na nchi yako?! Noh, this is not God!

Hakuna mtu anayekatazwa kutumia maneno ama nukuu ya waasisi katika nyanja yoyote ile ya kisiasa, kiutamaduni ama kimaendeleo. Lakini watanzania inatulazimu sasa tupime kwa mara nyingine uzito na matumizi ya maneno/nukuu za waasisi wetu. Ni muda muafaka sasa kwa watanzania wote kupima uzito wa kauli hizi mbili; "Wananchi wasipoyapata mabadiliko ndani ya CCM, watayapata nje ya CCM" na "Mtu yeyote anayekimbilia ikulu, muogopeni kama ukoma"!
Tukumbuke kuwa, hatima ya watanzania iko mikononi mwa watanzania wenyewe!
 
Kwa hiyo unatushaurije? Maana Lowassa ndiye habari ya mjini kwa sasa, upende usipende!
 
Tulia tulia kijana usihahe kama unakunya mlangoni. Ngoma inogile.
 
Kwa hiyo unatushaurije? Maana Lowassa ndiye habari ya mjini kwa sasa, upende usipende!

Ndo habari ya mji gani? Mtamuua mzee wa watu mkimfilisi, atabaki anadaiwa madeni mnamkimbia, anakufa.
 
Kwa hiyo unatushaurije? Maana Lowassa ndiye habari ya mjini kwa sasa, upende usipende!
Honolulu wewe utakuwa mvuta bangi,bado unaishi Kwa wazazi wako, una eliu ndogo sana, ni mwizi, ni muongo muongo, n.k., maana hujielewi.
 
Last edited by a moderator:
CCM hakuna msafi pale ni dhuluma kubwa kumkata Lowasa eti mchafu kuna msafi pale inanikumbusha andiko la Yesu kuwaambia jamaa walomkamata muhalifu akawauliza aliye msafi aanze kutupa jiwe wote wakatawanyika Watz tusikubali Tutawaliwe kwa kigezo cha Usafi RADA EPA ESCROW Chanzo ni CCM tupambane na propaganda nitampa EL kura yangu ili niwaonyeshe tu kuwa cpendezwi na majungu na chuki.EL kawakosea nin mpaka akatwe kama kuiba wote wezi.
 
Back
Top Bottom