Mungu nisaidie niione siku hii

Mungu nisaidie niione siku hii

MAKUNDA

Senior Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
115
Reaction score
39
Mungu Muumba wa nchi mwingi wa rehema. Wewe uliyeziumba mbingu na nchi nakuja mbele zako usiku huu nikiwa ninamzigo moyoni mwangu juu ya nchi yangu ya Tanzania ambayo uliiumba na kuipa kila kiitwacho baraka. Nakushukuru kwa jinsi ulivyoipendelea Tanzania. Kama ulivyowaumba malaika wako wema lakini akatokea muasi Lusifa, ndivyo nchi yetu Tanzania pamoja na baraka zote ulizoipatia kuna shetani mbaya aitwaye CCM ambaye anaifanya nchi ionekane Masikini na yenye kujaa dhuruma, uchoyo wa wenye madaraka huku wanyonge wakiumia na kunyanganywa hata kile wanachotafuta kwa macho. Eee, Mungu wangu nakusihi Katika Jina takatifu la Yesu Kristo wa Nazareti Unijarie kuiona siku ambayo Tanzania itakuwa haina CCM madarakani, naitamani sana maana kwa hilo naona matumaini ya watu kufufuliwa na kufaidi baraka zako ulizowabarikia. Nina umri wa miaka 52 kwa maisha ya mtanzania ninaekea jioni naomba maombi yangu yapata kibali chako ili siku hii ifike mapema wakati bado macho yangu yanaona.
Mungu wewe mwenyewe unasema kuwa hutoi nyoka badala ya samaki au nge badala ya yai hivyo naamini kuwa yamekuwa jina lako lihimidiwe. Walio na uchungu wa nchi hii jibu kwa kusema AMINA.
 
Eeee Mungu tujalie wanao ktk hili.

Tuepushe na kikombe hiki,tena kituepuke kabisa.
 
Pepo toka,Pepo toka nasema,hili Pepo la CCM lishindwe na litokomee kabisa kwa Jina la Yesu,Amen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom