Tatizo hapo tunalinganisha machungwa na ndizi, huwezi linganisha Marekani na China hata kidogo, historia na utamaduni wao ni tofauti. Mambo yaliyowezekana Marekani sirahisi kuyafanyika China.
Sirahisi kusambaratika na haya mambo ya kujua wanagharibi wanasema nini sio dili kwasababu hata wachina wakawaida wakijua Sen. Tom Coburn kasema nini haina tija kwa maisha yao kilasiku ni sisi wabongo tuu ndo huwa tunapapalikia mambo ya nje.
Hata Marekani kwenyewe vyombo vyote vya habari havisemi ukweli (vipo kipropaganda zaidi). Huwa hawatoi habari za uhalisia zaidi ya zile za kipropaganda juu ya mambo ya nje, Chaneli kama za aljazira, DW, Sky News, CNN international na BBC huwa hazipatikani kwenye chaneli za kawaida (abc, cbs, fox, news, mnsnbc n.k) ambazo zinatumiwa na wamarekani wa kawaida.
Taifa lolote kubwa haliwezi huwa hivyo bila ya kujenga utamaduni wa kuwapumbaza wananchi wake.Marekani inafanya hivyo pia, we angalia mfumo wa elimu ya msingi ya marekani utaona jinsi watoto wanavyokuwa brainwashed. Hawafundishi jiografia ya dunia kama sisi tulivyosoma bongo, hii yote ni kupumbaza jamii isijue chochote kuhusu nje ya Marekani ili iweze kutawaliwa. Mfano mzuri ni huduma za afya ya jamii, wamarekani wengi wameaminishwa kuwa gharama kubwa za matibabu nchini kwao ni kutokana na ubora wa huduma za afya binafsi lakini hii si kweli, Cuba jirani zao ambao matibabu yao ya serikali ni bure wanawazidi kwa ubora.
Sasa wamarekani wengi hayajui haya kwasababu hawapati habari hizi kwenye vyombo vya habari. Sasa unaweza kuniambia mbona Wamarekani wanaweza kupata haya kwenye mtandao? Tatizo ni kwamba kama hujui hata ukweli upi wa kuutafuta kwenye mtandao huwezi jua neno gani la ku-google.
Tunahitaji China na hata Afrika kama ikiwezekana ili kuwa na uwiano wa uongozi duniani, hata hiyo Marekani yenyewe wana sheria ya uwiano wa umiliki (sherman Antitrust Act) ambayo inazuia mtu/chombo kimoja kutawala kila kitu bila ya kuchunguzwa na serikali waliweka hii sheria kuzuia ukiritimba wa watu kama wakina Bill gates (software) na John D. Rockafellar(mafuta na chuma). Kwasasa wamarekani ni wakiritimba katika kila kitu, tunahitaji uwiyano katika dunia hii ya sasa.