Ni suala la wanamkoa na wanamajimbo yote kulishika hili,kwa jinsi navyoona in vyema mkatumia muda mwingi kujaribu kuwashawishi wagombea wote wa nafasi za ubunge wote wawe ni wakazi wa kudumu wa maeneo hayo,sina maana asiye mzaliwa hafai bali hakikisheni wanakuwa wana makazi yao ya kudumu,tuna bahati mbaya ya kuchagua watu wenye makazi yao nje ya mkoa na zaidi wanaoishi Dar,hawa watu kamwe hawatatusaidia kwasababu wanakuja jimboni kama sehemu ya kutembea ama likizo,wakati wa kuhitaji mikakati ya pamoja kuhusu maendeleo wao hawapo na wala haiwasumbui sana kwani wanajua siku chache zijazo kipindi kikiisha watarudi walikotoka maisha yaendelee na sie wananchi daima tutaachwa na matatizo yetu miaka nenda miaka rudi ...yangu ndo hayo kwenu ndugu zangu