JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 108
Chande: Tunaahidi uwazi na uadilifu kwenye uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa ‘Matukio ya Uvunjifu wa Amani’ wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othman, amesema tume imepewa jukumu la kufanya uchunguzi huru, wa kina na wenye uwazi ili kutoa majibu sahihi kwa Watanzania.
Akizungumza leo Desemba 1, jijini Dar es Salaam, ameainisha maeneo sita yatakayochunguzwa kuwa ni pamoja na chanzo cha vurugu, malengo ya waliopanga vitendo, madhara yaliyosababishwa, hatua zilizochukuliwa na Serikali, na mapendekezo ya kuimarisha uwajibikaji na utawala bora.
Jaji Chande amesisitiza kuwa lengo la Tume ni uponyaji wa kitaifa na aliwataka watu au taasisi zenye taarifa kuhusu matukio hayo kutoa ushirikiano. Tume imepanga kuwahoji wahusika mbalimbali ikijumuisha waathirika, watuhumiwa, vyama vya siasa, asasi za kiraia, wasimamizi wa uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), viongozi wa dini, makundi ya kijamii, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.
Aidha, akijibu maswali ya wanahabari kuhusu mgongano wa maslahi wa uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Stergomena Tax, katika tume hiyo licha ya kuwepo kwa tuhuma kwamba jeshi lilihusishwa na matukio ya ukatili dhidi ya waandamanaji, Jaji Chande alisisitiza kuwa uteuzi wa wajumbe ni mamlaka halali ya Rais na kwamba viongozi hao wanateuliwa kwa kuzingatia vigezo anavyoona vinafaa kisheria. Ameongeza kuwa, Tume itaanza uchunguzi upya kulingana na ushahidi wa kweli, ikiwataka wadau wote kushirikiana, na hata wale wanaokataa kushirikiana ikiwemo baadhi ya vyama vya siasa, kupewa nafasi kwa sababu mchango wao ni muhimu katika kuandaa ramani ya taifa kuelekea amani, maridhiano, na mapendekezo ya mageuzi kama Katiba Mpya.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wameendelea kukosoa uhalali wa Tume hiyo wakisema haina dhamira ya kutafuta kweli, wakihoji wanawezaje kuwahakikishia watanzania kuwa hawajapewa maelekezo ya jinsi ya kuchunguza ikiwa wameteuliwa na mtuhumiwa namba moja wa mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi? Lakini pia wataweza kwenda nje ya hadidu za rejea ikiwa ndio msingi wa uchunguzi wao? Pia wamesisitiza mtuhumiwa hawezi kujichunguza mwenyewe, na kwamba Rais Samia hakutakiwa kuhusika kabisa katika uundaji wa Tume hiyo ili kuhakikisha inafanya kazi kwa haki na uhuru.
Wengine wamesema tume hiyo imeundwa ili kuhalalisha NGO, wananchi na taasisi nyingine kupewa lawama ili wahusika waepuke kuwajibishwa kutokana na hadidu za rejea kuwaelekeza hivyo, lakini pia katika mambo sita waliyosema watayachunguza, hakuna walipotaja kuhusu kuchunguza aliyetoa amri ya kuwafyatulia risasi raia na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Wananchi wanaona kama Serikali inachukulia kuwa suala la mauaji halikutokea na watu walifariki kwa bahati mbaya kwenye maandamano.
Fr. Kitima awataka viongozi kukiri na kuwajibika juu ya mauaji ya raia yaliyotokea Oktoba 29. Asema mazungumzo yake na Waziri Mkuu hayakuhusiana na TEC
Akizungumza na vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, amesema kuwa Kanisa Katoliki linapotetea ustawi wa jamii, heshima ya utu na haki za msingi, halifanyi hivyo kwa maslahi ya binafsi bali kwa manufaa ya Watanzania wote. Amesema, maumivu ya wananchi yanatokana na kutokiri ukweli kuhusu mauaji wakati wa uchaguzi, akisisitiza kuwa waliokuwa na dhamana ya usalama wa wananchi ndiyo wanaopaswa kuwajibika badala ya kuwabebesha lawama watendaji wa ngazi ya chini.
Kuhusu madai ya raia kuuliwa, Fr. Kitima amesema Kanisa limekuwa shahidi wa majeruhi na miili ya watu waliopigwa risasi kupitia hospitali zake, huku baadhi ya askari wakiwazuia majeruhi kutibiwa na kutaka kuona miili katika mochwari, akiongeza kuwa hata wale waliokuwa wamebaki majumbani walifuatwa na kuuawa huko.
Alipoulizwa kuhusu madai vijana kununuliwa ili waandamane, Kitima amesema hilo si kweli na ni kuwakosea heshima vijana, akibainisha kuwa chanzo cha maandamano ni hisia za kutokuhisi usalama kutokana na utekaji, kupotezwa na mauaji yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili, akisisitiza kuwa matukio ya vifo, utekaji, majeruhi na uvunjifu wa haki za binadamu si mapya nchini.
Aidha, ameonya kuwa kupuuza sauti za viongozi wa dini ni hatari kwa taifa sababu walionya kuhusu uminywaji wa haki nchini pamoja na matukio ya utekaji lakini walipuuzwa akirejea ushauri uliotolewa na TEC Aprili 30 ambao uliwasilishwa serikalini Agosti 27, lakini tangu siku hiyo alipokea vitisho vya kuuawa. Amebainisha kuwa bado anaweza kuwa katika hatari kwa kusema ukweli unaohusu uhai wa watu na mustakabali wa taifa. Pamoja na hayo, Fr. Kitima amesema kuwa kunaonekana uwepo wa chombo kingine chenye nguvu kuliko Polisi ambacho kinafanya vitendo hivyo vya utekaji na kupoteza watu bila kudhibitiwa, na ndio maana matukio hayo hayakomi.
Kuhusu Serikali kusema kilichotokea kilikuwa ni vurugu pamoja na kutilia msisitizo kwenye uharibufu wa mali, Fr. Kitima amepinga kauli hiyo na kusema yale yalikuwa maandamo, akikiri kuwa kulikuwa na uharibifu wa mali na kusema kama jinsi Serikali walivyokiri kuhusu uharibifu wa mali ndivyo hivyo wanapaswa pia kukiri kulikuwa na mauaji.
Kitima aliongeza kuwa vijana walipata taarifa kuwa kulikuwa na maandamano, na ndio maana vyombo vya ulinzi nchi nzima vilijipanga kwaajili ya hilo. Amesema watanzania hawatamsamehe mtu mpaka waliofanya mauaji wakiri, na kwamba anayepaswa kuombwa msamaha ni watanzania wanaodharaulika kama wanyonge, na kama wasipoomba msamaha basi itawagharimu hata iwe miaka mia ijayo.
Kuhusu jitihada zinazofanyika ili kurejesha amani nchini ikiwemo kuunda Tume ya Uchunguzi pamoja na kufanya maridhiano, amesema, bila kukiri mauji kufanyika jitihada hizo hazina maana yoyote. Amesema, watu hawatakiwi kusubiri Tume kuchunguza na kuja kusema watu waliuawa ndio Serikali ikiri wakati wananchi wameshuhudia mauaji hayo kutoka sehemu mbalimbali, ni jambo ambalo lilitakiwa kufanyika mara moja pamoja na kusema nani alifanya mauaji hayo, kwasababu Watanzania wana akili na wanajua kilichotokea, kutokukiri na kusingizia hawajui kilichotokea wakisubiri majibu ya Tume ni kukosa unyenyekevu.
Aidha, amesema serikali haiwezi kuunda tume ya kujichunguza, badala yake inatakiwa kuhusisha watu na taasisi kutoka ndani na nje ya nchi ili kuondoa mashaka ya kujipendelea kama ambavyo walipendekeza katika tafakuri iliyofanywa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).
Mwisho Kitima aliwashauri vijana wasikate tamaa na wasimame kwenye ukweli, akisema na taasisi ambazo hazina maslahi kwenye uongozi iwashauri vijana ili kufanya maamuzi sahihi, na kwamba wahakikishe misingi ya uchaguzi wa haki inarudi nchini maana kipindi hiki kuna “Selection” badala ya “Election”, akitolea mfano wa wabunge walioshinda kwa asilimia 99, akisema hii inathibitisha kushuka kwa kiwango cha Demokrasia nchini.
Akizungumzia mazungumzo yake na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, Kitima amesema yalikuwa ya binafsi na si ya Baraza la Maaskofu, kwa kuwa hakupewa ajenda wala barua ya TEC.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamekubaliana na hoja alizotoa Fr. Kitima pamoja na kumpongeza kwa ujasiri wa kuzunguzia ukweli wa yanayoendelea nchini licha ya kuweka maisha yake hatarini hasa kwa Serikali isiyotaka kusikiliza ukweli kutoka kwa wakosoaji. Aidha, wamesema viongozi wa dini wanatakiwa kufuata mfano wa Kanisa Katoliki ambao wamekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya umma na kukosoa pale wanapoona Serikali haifanyi vizuri, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuleta uwajibikaji na kuhakikisha nchi inaendelea.
Wengine wameeleza kuwa hoja ya Kitima kuhusu Polisi kukataa majeruhi kutopewa matibabu na kulazimisha kupelekwa kwenye chumba cha maiti inaongeze ushahidi juu ya uhusika wa Serikali na vyombo vya ulinzi kwenye mauaji ya raia, wakitaka uwajibikaji ufanyike.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wameonyesha wasiwasi kuhusu usalama wa Kitima, wakidai kuwa safari hii Serikali inaweza kufanya shambulio baya zaidi dhidi yake kutokana na kuikosoa hasa katika kipindi hiki ambacho wanahitaji kuungwa mkono.
Rais Samia kuhutubia taifa Desemba 2, RC Chalamaila atoa wito wananchi kutoa taarifa za uvunjivu wa amani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Rais Samia atakutana na wazee wa mkoa huo Desemba 2, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC, ambako atatumia nafasi hiyo pia kuhutubia Taifa.
Amesema mkutano huo ni hatua muhimu katika mchakato wa kurejesha na kuimarisha amani nchini, ambapo Rais ataambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na wale wasiokuwa watumishi wa umma.
Chalamila pia ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa wanapobaini makundi yenye viashiria vya kuvuruga amani, akibainisha kuwa vikosi vya ulinzi vinaendelea kuwepo katika maeneo mbalimbali kulinda usalama wa mkoa huo akisisitiza kuwa ni wajibu wa wananchi kushirikiana na Serikali kuu pamoja na za mitaa kuhakikisha mkoa unabaki kuwa salama wakati juhudi za kuponya taifa zinaendelea.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamehisi huenda Rais Samia anaenda kumuagiza DPP amuachie Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ili mchakato wa maridhiano uanze na hivyo kupunguza na kuwashawishi vijana kusitisha maandamano yanayotarijiwa kufanyika Disemba 9.
Aidha, wengine wameonyesha msimamo wao wa kutotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kukamata wanaotaka “Kuvuruga amani” wakisema madai yao ni ya msingi na kuandamana si kosa kisheria, na zaidi hawawezi kutoa ushirikiano wowote kwa Polisi kutokana na mauaji waliyofanya wakati wa uchaguzi.
Patrick Lumumba ashauri Tundu Lissu kuachiliwa ili kurahisisha maridhiano ya Kitaifa
Mwanaharakati na mwanasheria maarufu kutoka Kenya, Prof. Patrick Lumumba, amesema hatua za awali zilizochukuliwa na Rais Samia ikiwemo kumuelekeza DPP kupitia mashauri ya vijana waliokamatwa kutokana na maandamano ya Oktoba 29 kwa lengo la kuyafuta ni ishara ya mabadiliko chanya, lakini hazijatosha kurejesha utulivu wa kisiasa nchini Tanzania.
Akizungumza na Diamond TV ya Zambia, Lumumba amesema hatua kubwa inayohitajika ni kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani Tundu Lissu, akisisitiza kuwa hilo linaweza kufungua mlango wa maridhiano ya kitaifa.
Prof. Lumumba ameongeza kuwa Rais Samia ana nafasi ya kihistoria kurejesha imani ya wananchi kupitia mchakato mpana wa maridhiano, ambapo ametaja hatua muhimu kama vile; kuwaachia huru wote waliokamatwa kwa sababu za kisiasa, kuunda tume huru ya kuchunguza matukio ya uchaguzi kwa ushirikiano wa wataalamu wa SADC na EAC, pamoja na kuitisha mkutano wa kitaifa utakaowakutanisha vyama vyote vya siasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wadau wengine kujadili mustakabali wa taifa.
Maoni ya wananchi:
Baadhi ya wananchi wamesema mjadala wa maridhiano haupaswi kuonekana kama suala la vyama vya siasa pekee, bali ni sauti ya wananchi wanaotaka mageuzi ya msingi kama Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na kusitishwa kwa vitendo vyote vinavyokiuka haki za binadamu.
Aidha, wengine wamesema hakuna maridhiano au majadiliano yoyote yanayoweza kufanyika kabla ya uwajibakaji kwa wote waliohusika kuwaua raia wakati wa maandamano.