Mugabe amsifia Trump kwa kuzuia wahamiaji wasiingie Marekani

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Rais Mugabe ametoa sifa kemkemu kwa rais mpya wa Marekani Donald Trump akisema
"Trump anahitaji kupewa muda ili awafanyie kazi Wamarekani waliomchagua".

Akizungumza na vyombo vya habari rais Mugabe alinakiriwa akisema, Trump amefanya vizuri sana katika nia yake ya KUZUIA WAHAMAJIAJI haramu kuingia Marekani.

Mugabe aliendelea kusema
MAREKANI ni kwa ajili ya WAMAREKANI. Na akaongeza kusema pia hata
"ZIMBABWE ni ya WAZIMBABWE".
Hivyo wasimlaumu Trump kwa nia nzuri aliyo nayo bali wamuunge mkono.
Chanzo: CNN
 
Ukiwa na Viongozi kama trump na Mugabe ni rahisi dunia kuingia kwenye vita kwasababu kila mmoja anaona nchi yake ni bora. Kusema Zimbabwe ni ya wazimbabwe tu au nchi flani ni ya watu flani ni kueneza ubaguzi na chuki.
 
Hebu tueleze chuki ipo wapi hapo?
Yaani unatuambia kuwa unataka kwetu pawe kwenu pia!!!
Acha kuandika ujinga kipambavu namna hii.
 
Sio kwetu pawe kwenu ila haileti picha nzuri akimwambia mgeni kwamba hii sio nyumba yake (japo ni kweli). Watu kama mugabe ni wabaguzi na hawapendi kuona nchi ina wageni ndio mana alichukia sana kuona mtu mweusi kama Obama anaitawala nchi ya wazungu.
 
Kaa kwenu achana na fikra za Vasco Dagama.
Hii sio millennium yake.
 
Huyu mzee si kwamba anajipendekeza hasije Trump akamkomalia shingoni. Nimepita Zim karibuni yaani ni shida. Benki unaruhusiwa kuchukua dola hamsini kwa siku. Kumbuka wanatumia US $ baada ya pesa yao kutokuwa na dhamani. 90% ya wazimbabwe hawajaajiriwa. Mzee has reduced his country to nothing. The only people enjoyed there are wakuu wa jeshi na walio karibu na mzee. Anatawala kwa mabavu kwa kutumia wanajeshi. Zim wana hali mbaya sana.
 
Ukiwa na Viongozi kama trump na Mugabe ni rahisi dunia kuingia kwenye vita kwasababu kila mmoja anaona nchi yake ni bora. Kusema Zimbabwe ni ya wazimbabwe tu au nchi flani ni ya watu flani ni kueneza ubaguzi na chuki.
Hamna ubaguzi hapo ni ukweli. Na ndiyo maana kwenda nchi nyingine unahitaji visa na unapewa muda maalum. Otherwise, majina ya nchi yafutwe na visa ziondolewe
 
Ukiwa na Viongozi kama trump na Mugabe ni rahisi dunia kuingia kwenye vita kwasababu kila mmoja anaona nchi yake ni bora. Kusema Zimbabwe ni ya wazimbabwe tu au nchi flani ni ya watu flani ni kueneza ubaguzi na chuki.
Unataka uturudishe kule kule........Kwamba ukiwa na kazi mbili zakufanya basi unamgawia mwenzako moja,,yaani kwangu kuwe kwako,,,...
 
Back
Top Bottom