Muda unafika ndipo jamii ya siasa Tanzania itameguka na kutoa fursa ya utawala mpya

Alper

Member
Mar 20, 2017
18
4
Hapa nazungumzia vitu rahisi sana ambavyo kwa tafakari halisi vinaleta maono mapya kwa ujumla kuhusu siasa ya nchi yetu na mabadiliko shitukizi ya kiutawala ambayo kimsingi kiini chake yanatokana na Dira ya siasa ya nchi.

Mfukuto wa joto kali uliopo kwa Watanzania hususani unaohusu milango mbalimbali ya kihisia, unatoa mwanya wa minong'ono ambayo inaashiria Watanzania kukosa furaha sana na nchi yao, japo wanaonekana kujikaza kama Sabuni ila muda unafika ndipo jamii ya siasa ya Tanzania itameguka na kutoa fursa ya utawala mpya kuazia ngazi ya chini kabisa yaani familia hadi ngazi ya juu ya kiutawala yaani kupitia mihimili mikuu mitatu ya nchi(Mahakama,Bunge na Serikali kuu).

Utashituka sana pengine baada ya kutaja mihimili mikubwa hiyo ya nchi, usishituke kwa sababu na kukumbusha kuwa mihimili hiyo yote pia inaongozwa na watu walio beba hisia tofauti tofauti kama jinsi ilivyo ngazi hizi za chini ambavyo sambamba watu ndio wanaziongoza.

Hisia hizo zote tofauti tofauti za Watanzania zinatokana na kauli za kujengea hofu miogoni mwao ambapo zinafaida kubwa sana katika kuleta mabadiliko ya kiutawala maana hutoa mazao mabaya zaidi yenye msingi wa kumbadilisha mtu kifikra, kuchoka, kuzoea na kutohisi jipya kiutendaji hivyo ndipo maazimio Mapya hujengwa mioyoni yanayoleta mabadiliko ya kweli kiutawala.

(Mfano mdogo sana rejea nchini Kenya wakati palitokea meguko la kisiasa kwa chama tawala KANU).Matunda yake yalileta mwanga mpya wa utawala mpya wa wakenya.

Hivyo basi Watanzania wenzangu nawasihi kukaa mkao wa kula kupokea utawala mpya wa nchi hii utakao leta zama mpya za furaha kuu kwa Watanzania wenyewe ifikapo hasa katika chaguzi kuu za nchi.

Nimeyanena hayo kutokana na kile nachokiona kinaendelea katika nchi hii, ambapo vinanipa furaha ya kuona utawala mpya unao kuja mda mfupi tangu uhuru wa nchi, maana matukio yote hayo yanaakisi nuru ya Watanzania kugeuka kifikra kuanzia ngazi ya chini hadi juu. Na kufanya kweli ifikapo 2020 kwa kutumia kura yao vizuri.

Asante.
 
Umeandika kiufundi Mno. .

Toka jioni ya siku alipoapishwa Amani ilitoweka mioyoni mwetu.

Ila trust me, tukimfukunyua atareact vibaya Zaidi, Kikubwa ni kumuachia Mungu tu.
 
Tatizo lake anafikiri akitumia nguvu ataacha legacy kama nyerere kumbe mwenzie alikua anatumia akili!

Hiki kizazi cha sasa ni korofi tofauti na miaka hiyo......
Eti hakuna mtu aliyenisindikiza kuchukua fomu hivyo hakuna wa kunipangia!

Amuulize wasira alivyosema jimboni kwake hata msipo nipa kura wake zenu watanipigia nini kilitokea mwaka 2015......
 
Back
Top Bottom