mgeni wenu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 3,664
- 1,730
Ngwangaluka Rais, mwamisha mohla,Safari ya kujagha ku maendeleo Doho Mchezo.
Mh Rais kwa kuwa umejua huko nyuma mambo yalikuwa hovyo sana,na kwa kauli yako mwenyewe umesema ni hovyo kweli kweli,nadhani huu ni muda muafaka sasa wa kuanza kufuatilia mauaji ya Raia wasiokuwa na hatia hasa wapinzani wa awamu ile kisiasa.
Watu walipewa kesi za ugaidi,wengine waliteswa na kuuwawa na wengine kupoteza viungo na mali kwa ajili ya waliopita.Nimefuatilia historia yako wewe ni mcha Mungu na umepata malezi mazuri ya kidini kwa Askofu mmoja pale Shinyanga ambae sasa ni marehemu (Aloysius Balina) sina shaka na imani yako japo madaraka hulevya.
Watanzania wenzako wamekuwa wakilalamika kubambikwa kesi na askari,huku nyuma wakiacha familia zinateseka na kukosa elimu na kupewa hakikisho la kufa maskini,huku wanaowabambika wakishindana kununua mali za wenzao kwa minada.
Nakuomba sana ni muda muafaka sasa wa kufuatilia mateso ya Watanzania wenzako, kama kuna watu walifanya hayo waanze mapema kujiondoa kwenye nafasi zao,ipo siku kwa imani ambayo watanzania wanaijenga kwako wataanza kuwataja hadharani na ikifikia hapo basi wakubwa wao ambao hawakuchukuwa hatua stahiki watumbuliwe kama ilivyokuwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Unda team ya kupita kila gereza ushuhudie mahabusu wanavyoteseka kwa makosa ya kubambikwa zamani, maombi unayoyahitaji tukuombee watesekao watakuombea mara dufu kuliko siso tuliopo uraiani,nakuomba sana. Kuna watu wamebadilishiwa mashitaka kutoka uzembe na uzururaji hadi mauaji.
Hili jambo limekuwa la kawaida kabisa.Vyombo vinajua ila havikuwa na mtu muafaka kwa muda muafaka, ile yema ya Doria mitandaoni najua wata print uzi huu na kumpelekea mkubwa wao.
Na kwa kuwa wewe unasoma humu kila jambo unalichukulia kwa uzito wa pekee, basi angalia leo jeshi letu linashindwa kutii bila shurti,mkataba wa fedha za kodi zinapigwa danadana.
Kwa heshima kubwa sana ni vizuri ukaomba tu viongozi wa Wizara na jeshi wakaachia nafasi zao hasa kwa ubadhilifu huu.Kuna askari wadogo wanaishi kwa shida sana huku wakubwa wao wanakula mabilioni. Hii imeleta chuki hata bana yao.
Kama kiongozi mkubwa katika taifa sio tu iwe sifa kwako ila onesha dhamira ya kile tunachoelezwa kila siku.
Mwisho kabisa sitaacha kukukumbusha suala la Meya wa jiji letu la Tanga.
Wabheja sana Bhagesh.