McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Wakuu,
Mkuu wa Majeshi Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ameibua mjadala mkubwa baada ya kuandika ujumbe kwenye mtandao wa X akidai kuwa ana mamlaka ya kumzuia Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, kushiriki tena katika chaguzi za Uganda.
Kupitia ujumbe huo uliowekwa mtandaoni Januari 22, 2026, Kainerugaba alisema kuwa haijalishi kama Kyagulanyi yupo ndani au nje ya nchi, yeye kama CDF anaweza kumzuia kushiriki shughuli zozote za uchaguzi kwa kile alichokiita maslahi ya usalama wa taifa na manufaa ya nchi.