Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Tasnia ya filamu Tanzania(Bongo Movie) inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kung’ara. Safari hii mtoto wa kitanzania aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant Story.
Filamu hii inajaribu kuonyesha jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa. Evan anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan; Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama bibi yake Evan na wengine wengi.
Pamoja na kucheza filamu hiyo pia Evan amefanya audition nyingi kwa hiyo Mungu akipenda ataonekana kwenye matangazo ya kibiashara na filamu nyingine nyingi zaidi.
Source: Dewji Blog