Mtoto wa Kawawa atumia jina la Baba yake kunyanyasa Wawekezaji, asaidiwa na Uhamiaji na TRA

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397


Kwa mujibu wa hii video, Mwekezaji raia wa Denmark analalamika kuhujumiwa na Mtu aliyemtaja kuwa ni Twaha Mfaume Kawawa.

Jamaa aliwekeza kwenye sekta ya kilimo kwa miaka 5 na kuajiri Watanzania, anakiri walifanya kosa kubwa kukubali kuwa na ubia na Mtanzania.

Mtoto wa Kawawa alitaka kugombea hivyo akaomba fedha kutoka kwenye Kampuni lakini walipomkatalia alichukua hela kwa nguvu

Walipoona amekuwa tatizo walimuomba arudishe hisa alizopewa bure kisha alipwe Milioni 8. Anaeleza kuwa ametumia jina la Kawawa kupenya Uhamiaji, Mahakamani na TRA kumhujumu mwekezaji huyu.

Mwekezaji huyu anaomba msaada wa Rais Magufuli ili aweze kurejea na kuuokoa mkopo wake aliouchukua kutoka benki moja huko kwao Denmark.
 
Nimeipeleka mahala husika Nadhan ataipata mheshimiwa Magufuli

Watoto wengi baba zao wenye kufahamika, hutumia majina ya wazazi wao kuwatisha na kuwahujumu watu. Nadhani kuna umuhimu wa kuthibiti ufisadi huu kwa kuwapa kibano kikali wahusika!
 
nahisi wewe haijakuuma aiseeee nimeumia mbaya mzungu wa watu mpaka kiswahili anajua ....walai naenda mtumia mpaka account ya msemaji wa ikulu insta .......hatuwezi chafuliwa kiasi hichi na mjinga aliechoka maisha
Jamaa anasema anaweza kuwashawishi wawekezaji waondoke nchini lakini haoni kama ni busara
 
Back
Top Bottom