Mtoto anataka kumjua baba yake

Mtoto anataka kumjua baba yake

Big Lion

Member
Joined
Jan 5, 2015
Posts
46
Reaction score
15
Ni ndugu yake na pia ni dada yake mkubwa. Baba yao alimuoa mama yao akiwa na tayari na mtoto wa kike ila alikua mdogo sana hivo baba alikubali kumlea mtoto hivo mtoto katika kukua kwake alijua yule ndo baba mzazi wake. Amemsomesha hadi kamaliza form six.

Kaka mdogo wa huyu dada ambaye kamaliza form 4 yeye alishaambiwa na baba yake kuwa dada hamjazaliwa pamoja ila iwe siri yake kwan dada akijua hilo atataka kumjua baba yake ni nan.

Hivi majuzi kaka akatoroka kaiba gari ya mzee kaenda kujirusha ila dada akastuka dogo kaiba gari so akasema kwa baba. Ikawa bifu kati ya dada na kaka sasa.

Wakaanza kutukanana kwa sms. Sasa kaka kamfungukia dada yake kuwa
"kwanza hapa sio kwenu tunakutunza tu. Gari ya baba angu inakuhusu nn"

Ishu imekua kubwa sasa mtoto anataka kumjua baba yake na anadai alishasikia muda kwa watu wa nje kua yule sio baba yake but hakutilia maanani.

Mbaya zaidi baba yake halisi huyo dada naye ameoa na anafamilia yake ila wakibaatika kuonana mama anamtambulisha kuwa huyu ni mjomba.

Sasa dogo kaja kuniomba ushauri home anaogopa kwenda maana mama anajua yeye ndo kaharibu.
 
Walikosea kumwambia huyo mtoto wa kiume kuwa huyo binti sio dadaake wa damu kwasababu nae ni mtoto na akili za kitoto matokeo ndo kama hayo sasa wangesubiri apevuke.Sasa inabidi huyo binti aelezwe ukweli tu kuhusu biological father coz wakiendelea kuficha atajua tu haliepukiki!Maji ndo yashamwagika tena hayazoleki na mama apunguze hasira hata kama kijana kasema NI UKWELI!
 
Baba huyu nae mnafiki tu. sasa kwanini alimwambia mwanae kua huyo si dadake wa kushea baba. kama waliamua kuifanya siri basi ni bora angenyamaza kuliko tafrani alotengeneza. huyo dogo aende tu nyumbani akaombe radhi hakuna suluhu nyingine. na wazee waseme tu ukweli. bint wa form six mbona mkubwa tu anajielewa akiambiwa ataelewa tu
 
Walikosea kumwambia huyo mtoto wa kiume kuwa huyo binti sio dadaake wa damu kwasababu nae ni mtoto na akili za kitoto matokeo ndo kama hayo sasa wangesubiri apevuke.Sasa inabidi huyo binti aelezwe ukweli tu kuhusu biological father coz wakiendelea kuficha atajua tu haliepukiki!Maji ndo yashamwagika tena hayazoleki na mama apunguze hasira hata kama kijana kasema NI UKWELI!
Everything happens for a reason....:smile-big::smile-big:
 
Huyo Baba naye hana kaba ya ulimi!!!
Mama akubali tu kuwa wakati umeshafika wa kuwa mkweli kwa bint yake.
 
Inaweza Kua ni rahisi kusema kua, ingekua mimi nigetaka kujua tuu ukweli kama Huyo alonilea ni Babaangu kweli Au laa, baada Ya hapo nikujua jee biological dad Anajua kua mimi ni mtoto wake? Halafu ningeendelea na maisha..
 
Ilitakiwa iwe hivyo ili maandiko yatimie japo si kistaarabu lakini ukweli umebainika mpe pole dogo hii ndio dunia kuna mengi.
 
....hivi kuna mwanadamu mwenye uhakika kuwa mwanaume amuitaye baba ni baba mzazi?

...mwambie huyo rafikiyo kama ana dukuduku lolote amalizane mamaye
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom