MTOTO AMCHINJA BABA YAKE MZAZZI!

Lipijema

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2015
Posts
953
Reaction score
1,540
Huku ndiko Dunia yetu inapokwenda kwa sasa! Huyu mzazi si mwenye kipato kikubwa ni mwenye hali ya kipato cha kawaida sana. Anaitwa mzee OJOHI MASINA mzaliwa wa Utegi, ni mkazi wa Kambi hii ya Uvuvi Migongo Maisome na mwanawe anaitwa anaitwa Baraka Ojohi Masina. Mtoto huyu yasemekana siku ya juzi tarehe 19/10/2018. Alitumia panga kwa kutenganisha shingo na kiwiliwili cha Baba yake mzazi huko kwenye pori la Isinde Maisome wakiwa kwenye shughuli za kuuandaa mkaa kwa minajiri ya kujipatia kipato chao cha kila siku. Mtuhumiwa Baraka Ojohi alikamatwa na wananchi tangu siku ya tukio ambapo alitenda tukio hilo muda wa majira ya saa tisachana. Tunashukuru Jeshi letu la Polisi kwa kuwahi kufika kwenye tukio hili, walifika na kufanya uchunguzi huko polini na wakafika hapa Migongo kambini na kumchukua mtuhumiwa. Kwa sasa mwili wa marehemu umeletwa kwenye mji wake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
 
Mtihani huu
 
Sababu ya kumuua mzazi wake ni nini??
 
Hivi mko serious au ndio chai ya asubuhi mtu anaus mnasubiria polisi waje kumchukua akiwa mzima

Angechinjwa na yeye afe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…