Habari za jioni,
Kuna hii habari niliyokutana nayo leo kwenye gazeti la Mwananchi, kwamba mama amejifungua mtoto hospitali na baada ya kupata fahamu vizuri, anaulizia mtoto wake anaambiwa amefariki.
Anaulizia maiti ya mtoto, wanamwambia wameshazika. Kuulizia kaburi, akazungushwa zungushwa wee mwishowe ndo wanakuja kumpatia hiyo maiti
Mimi binafsi najiuliza;Je kuna mchezo gani kachezewa huyu mama? Kwa nini wadanganye washamzika mtoto wake alafu baadae waje kumpatia maiti?
Na je tutawaamini vipi manesi na madaktari wa sampuli hii? Na tutakuwa na uhakika gani kwamba kweli maiti aliyopatiwa ni ya mtoto aliyemzaa?