Mtindo Wa Maisha Uliokosa Utii Mbele Za Mungu Utazaa Jambo Baya Kwa Mtu

Mtindo Wa Maisha Uliokosa Utii Mbele Za Mungu Utazaa Jambo Baya Kwa Mtu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Yer 6:19 SUV
[19] Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.

Maisha ya watu wa Taifa la Yuda, vile walienenda, vile walifanya maamuzi yao vibaya hukumu ya Mungu iliwajilia juu yao, halikuwa tukio la ghafla, yalikuwa ni matunda ya maisha yao mabaya waliyoishi.

Hii inaonyesha kuwa Mungu anapotuagiza tuenende katika njia fulani, alafu tukaiacha hiyo njia na kugeukia njia nyingine mbaya, hukumu yake itakuwa juu ya kila mmoja aliyeenda kinyume naye.

Mungu wetu hutoa hukumu ya haki, kama alikuagiza kupitia neno lake uishije, ukienda kinyume ujue utahukumiwa kutokana na njia mbaya uliyokatazwa na Mungu ukaifuata.

Mataendo mabaya ya uasi, ibada za sanamu, dhuluma mbaya, na kiburi, ni mambo yanayosababisha tukutane na adhabu ya Mungu kama tulivyoona kwa taifa la Yuda.

Dhambi zetu huanza moyoni, haitokei ghafla mtu akaanza kumtenda Mungu dhambi, matendo mabaya na yaliyo kinyume na Mungu huanza kuumbika ndani ya moyo wa mtu, ndio maana katika kitabu cha Zaburi inasema;

Zaburi 119
11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

Mioyoni mwetu ndipo chanzo kikuu cha kuanza dhambi tunazozifanya kwa nje, ndio maana mtu aliyegundua chanzo cha kumkosea Mungu kipo wapi atakuwa na bidii ya kujaza moyo wake neno la Mungu.

Uasi wetu mara nyingi sio kama tunaufanya kwa kutokujua, kama tunavyoona kwa taifa hili, walifanya mambo mabaya kwa makusudi wakijua Mungu wao hapendi wanachofanya. Ndivyo ilivyo hata leo, watu wengi hupuuza sauti ya Mungu na kufanya mambo yaliyo machukizo mbele zake.

Kukataa kutii neno la Mungu linavyotuelekeza namna ya kuishi na kuenenda, ni kuasi mamlaka ya Mungu au maagizo yake, na madhara ya kumwasi Mungu ni makubwa kwa kila mtu aliyeasi.

Tunapaswa kuwa makini, tusije tukawa tunatembea kama vipofu wanaoelekea katika hukumu ya Mungu pasipo kujua wanaenda kuangamia. Tukishajua tumetoka nje ya mstari wa Mungu, hatupaswi kuendelea kubaki katika eneo la uasi, tunapaswa kuchukua hatua haraka kumrejea Mungu kwa toba.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom