Mtikila atishia kumshtaki AG

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,848

Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila

Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ameahidi kumfikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Jaji Fredrick Werema kwa madai ya kushindwa kuandaa muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, ili kuruhusu mgombea binafsi.

Mchungaji Mtikila alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema Mahakama Kuu ilishatoa hukumu iliyoruhusu kuwepo mgombea binafsi, lakini serikali ilikata rufaa ikipinga.

Hata hivyo alisema rufaa iliyokatwa na serikali haitengui hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.

Alisema hivi sasa serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) inaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu bila ya kuweka mazingira ya kuwepo mgombea binafsi.

"Hili suala si la hiari bali ni kitu kilichoamriwa na mahakama, hivyo hapa hakuna hiari bali serikali ilitakiwa kutekeleza," alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
peleka mahakamani hao mtikila, tunataka mgombea binafsi sisi...sijui wanaogopa nini hawa ccm...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…