Mtikila akamatwa...

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,656
Reaction score
37,821
Kwa wale wapenzi wa Rev chriss ama christopher mtikila kwa walioangalia ITV Kwa huzuni kubwa jamaa wakiwa na defender wamemnyaka na suti yake town na mikanjanaja yake kwenye mabegi na kuelekea kutmikia miezi yake kadhaa 6 huko jela

Kwa huzuni kubwa wapenzi wa uraiani tutammiss rev mpaka mafuta wa bwana alikuwa akisumbua mahakama zote za dar es salaam mpaka mwakani mwezi wa pili yaani 01/02/2011 bila matumaini na kwa huzuni kubwa inaonyesha jamaa atapigia kura akiwa jela kwa hukumu hii

Mungu amtie nguvu kama alivyoomba polisi aseme neno moja kabla ya kwenda kwenye gari la defender nasema haki aipo nchi hii na ipo siku haki ya mtanzania itapatikana hata kwa nguvu...naamini ipo siku tutaonana na kucheka upya kwa ajili ya uchaguzi wa 2015
natumaini sheria imefatwa mkondo wake naomba tuzidi kujipa moyo tuko na wewe kimwili na kiroho...hata baibo inasema tuheshimu mamlaka ya nchi atuna budi kufika wakati kuheshimu sheria za nchi pia

Mungu akubariki Rev chriss
 
mkuu kibonde jana ulimzunguzia kweli chriss ana nini anawasumbua mahakama hivi..ujawahi kuona hukumu ati hakimu anasema alie mfikisha mahakaamani alipe lakisita za kumtunza jela ..hata sisis tulishangaa ila nahisi yule mama amechoka bora azitoe na kama kweli ametoa naomba takukuru mmmhoji huyu hakimu yawezekana lakisita zinaingia mfukoni mwa watu baada ya kushindwa kukatiwa na REV CHRISS LIVE...

Kwa hili nakupa hongera kwa kukomaa na akimu kabla ya sheria kufwata mkondo wake....pole sana huko ni nyumba ya kila mtu ni muda tu ukifika mhusika atahoji yuko wapi..na sie tulio uraian tuheshimu mamlaka ya nchi ipo siku watu watakusikiliza wakisema basi imetosha hata jela yawezekana hutofika...kila la kheri..kibonde jamaa wamemnyaka bwana live na suti yake jana nilikutumia kama uko na kipindi leo umwambie mzee ajitayarishe na vkikorombwezo vya jela asije akashangaa wanamdaka maskini sijui ilikuwa ndoto ...nilitafuta namba ya chriss nkaikosa..tulilona hili
Pastor chriss
 
Sasa wewe Samsoni, Mtikila kashitakiwa kwa kosa la kudhulumu pesa ya mtu ulitaka asifungwe? Hapo aliyedhulumiwa angekuwa ametendewa haki? Kama angeshitakiwa kwa makosa ya kisiasa tungesema amenyanyaswa, lakini hili la kushindwa kulipa deni la mtu, hilo kwa kweli siwezi kusema lolote kwa kuwa sielewi ni haki ipi unayoipigania wewe ambayo anatakiwa kuwa nayo Mtikila na si aliyedhulumiwa pesa.
 
Mimi mbona tuko pamoja na ndio maana nimemtakia kila la kheri nilicholalama kama ulisikiliza matokeo ya kesi akimu alisema mtikila ataenda ndani miezi sita na ktk miezi hiyo mlalamikaji atatakiwa kulipa sh lakisita laki kila mwezi
na mtikila atakamatwa tu pale mlalamikaji atakapolipa lakisita..hilo ndilo lawama yangu je nisiye na hela siruhusiwi kupeleka muhalifu mahakamani nikiogopa kudaiwa hela ya chakula
 

Jamani mwenye full story aweke hapa kwa faida ya wadau.
 

Sheria za kumfunga mdaiwa wa fweza ilifutwa USA miaka ya 1800. Nchini Wingereza huwezi kufungwa kwa kudaiwa fweza sisi hii sheria ya kumfunga mtu anapodaiwa mpunga tumeitoa wapi na imeanza kazi lini? Je hii ndiyo sheria ambayo inafuatwa au ni kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi bora asweke ndani asichafue hali ya hewa?
 


Ungefanya utafiti yngalijua kuhusu hii sheria. Ipo na inafanya kazi si kwa huyu Mtikila bali kila mtu. Kama USA na UK imefutwa, ndiyo maana tuna dai katiba mpya ili tuondoe yasiyofaa. Hivi unajua kuwa kuna sheria inayoweza kukufunga ukipiga kelele[kama muziki] katika jamii!!! Ipo, lakini inahitaji mtu makini.
Mt alishitakiwa na mtu binafsi, amekiri deni, amepewa option alipe au aende jela. Sasa wewe unadhani haki ya Paskazia itazuiliwa kwasabau mtikila anagombea urais.
Msikae mbele ya key board mkaanza kuandika msiyoyajua.
 
Na yule mama waziri aliyemtapeli mwenzake na kupatikana na hatia mbona bado anatinga uraiani?
 

uwe unasoma sheria na kuzielewa vyema...ni sahihi alivotoa hukumu huyo hakimu..yes mshtaki anaweza kuamriwa kulipa hela za kumtunza mshtakiwa akiwa jela
 
funga mpuuzi huyu,ni tishio la amani kwa nchi nzima na siasa zake za gabachori.
 
Mimi naona haina maana hata kwa huyo mdai kwani bado haki yake hajaipata na bado ataendelea kutoa hizo pesa kwa miezi hiyo sita,kuna haja gani ya kumfunga mtu wakati ana vitu?Si wangeuza vitu vyake kufidia deni?Kwangu mimi ninaona bado haki haijatendeka labda tu kama mdai alitaka kumkomoa UNCLE SUSPENDER.
 
Yule Mzee mbishi kama alipewa option ya kulipa au ndani..akakomaa...
Hayo ndo matunda ..sema tutamiss vituko hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi..
 
Tatizo lakumfunga mchungaji siyo deni!ni adhabu,moja kudharau mahakama,2 kutohudhuria mhakama kwakipindi chote cha mwenendo wakesi!!Ndiyo maana hakimu akatoa adhabu ya kwenda jela nakulipa deni!Hivyo jeuri yake ndiyo imemfunga!!kwani alistahili kufungwa mwaka mmoja jela kwakosa lakushindwa kulipa deni.:A S thumbs_up:
 

Kwa nini nifanye utafiti ninapouliza swali rahisi kama hili? Utafiti gani huo ambao natakiwa niufanye wakati nipo kwenye blog ambapo I know for sure the answer is simple and known by others instantaneouly? Unasema tusikae kwenye keyboard na nani? Inaelekea unakaa kwenye key board na group lako la wapambe khe khe khee. Pengine tukurudishe gumbaru maana inaonekana umekurupuka. Mimi nimeuliza swala kwamba hii sheria tumeitoa wapi na imeanza kazi lini. Kutokana na kumbukumbu zangu tangu tupate uhuru sina kumbukumbu zozote za raia aliyefungwa kwa kuwa mdeni. Kama wewe unaifahamu hii sheria unachotakiwa ni kuiweka hapa na sio kutoa u-loafer wako.

Mtikila pamoja na manjonjo yake hata kama alimdharau Hakimu au mahakama angeswekwa ndani kwa kosa hilo na si kosa la kutokulipa deni. Akitoka kutumikia kifungo hicho unataka kutuambia kwamba deni la millioni 9.8 litakuwa sawa na hiyo adhabu? Au anatakiwa bado alipe? Na Je akilipa baada ya kutoka utawezaje ku-compensate muda wake wa kukaa ndani?

Sheria za pakashume hazitakiwi kutumika katika nchi ambayo inajisifia kwamba inafuta utawala wa sheria. Labda nikukumbushe japo kidogo tu kwamba -kuna waziri ambaye hakufungwa kama Jasusi wa JF alivyosema, Kuna Mafisadi kadhaa ambao ushahidi upo wa wazi ambao bado wanapeta kama Waziri aliyejisifia wakati flani kwamba ana vijisenti tu kule Jersey au Mkono jinsi alivyotajirika na fweza za BOT au Mkapa alivyofanya biashara Ikulu na kudhulumu Kiwira au mkewe jinsi alivyojitajirisha kwa njia haramu na nyumba za NHC etc.

Whether you like Mtikila or not sheria ni lazima zifuatwe na ionekane haki inatendeka iwe kwa muuza machungwa wa Kariakoo ama mwanachama wa Chama Cha Majambazi.
 

Khe khe kwa hiyo hapa unatuambia kwamba hakimu alikuwa emotional ... if that was the case hafai kuwa hakimu.
 

Wengi wanakurupuka kuponda tu, bila kujua undani, hata huyu aliyeleta hii habari amelete kiumbeya zaidi wala haikukamilika, tayari watu wameanza kuhukumu, wameanza kuzomea, ni aibu iliyoje, kumbe chungaji kafungwa kwa kusa la kudharau mahakama na wala si la madai, kwani kaambia alipe dena. Inawezekana hata ile mil 3 ya Rostam hajalipa, lakini hatafungwa kama atapelekwa mahakamani, ila ataamrishwa kulipa tu, ila akidharau mahakama atahukumiwa kwenda jela na dani litabaki palepale. Nashukuru, imekuwa ni funzo kwetu, hatutakurupuka kujibu, kuhukumu na kutukana hoja bila ya kupata undani wake, tumejifunza na hatutarudia tena, tutakuwa wanafunzi wasikivu. MWISHO, POLE SANA MCHUNGAJI LAKINI HUWEZI JUA MUNGU AMEKUEPUSHA NA NINI. UCHAGUZI WA TARIME, CHADEMA WALIKUPIGA MAWE, NA UKATOKA DAMU, NDIYO UKAMWAGA DAMU, HATUJUI NI NINI KINGEKUPATA SASA HIVI KWENYE UCHAGUZI UJAO. HUENDA MUNGU KAKUEPUSHA NA MENGI. NABII YUSUF ALIPOKUWA ANATAMANIWA NA MKE WA MFALME ALIONA NI AHERI YA JELA, SO NO ONE KNOW.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…