Ukiona hivyo, watoto wao jamaa hao wa wizara hawasomi shule hizo. Huwezi kufanya kitu kama hicho kwa kujaribu ati kama kisu hiki kinakata kweli au kinachoma, kwa kurudia kisu kilichokujeruhi juzi. Wasitufanyie kiini macho hawa. Kama wizi wanaufungulia wenyewe kwa kuwapa watoto wao, au la kama wamo watoto wao basi huenda wamewapa maswali hayo watoto wao ili walio hohehahe wafelishwe.
Wanapima skills au wanapima uwezo wa kufaulu mitihani? Ni kitu cha kawaida mtu kujiandaa kwa kufaulu mtihani, ukijaniuliza baadaye swali lilelile baada ya mwezi usidhani nitajieleza kama nilivyokueleza wakati wa kwanza, kwani mtihani ukiisha na akili yangu naibwaga ipumzike. Kuna mtu anachekelea kufanyishwa mtihani?
Ufisadi mwingine huu, wanatafuta namna ya kuitafuna fedha ya wananchi kwa kisingizio cha utafiti wa kufanyisha watoto mitihani. Ukiuliza wametumia kiasi gani usishangae wakikuambia Bilion nne. Mbona wizara hiyo hiyo imeshindwa kuwashikisha adabu walimu wanaoiba pesa ya wazazi kwa kusingizia mia mja ya mtihani kila siku na mia tano kila weekend kwa wanafunzi, na mtoto asiyetoa pesa hiyo hulambishwa njiti, na DSM hapahapa? Hawaoni hilo?
Leka