Nina rafiki yang 1 alikuwa na mpenzi wake alidumu naye takriban miaka 2, jamaa alimpenda sana demu udhaif alioutumia demu kumnyanyasa jamaa kimapenz kwa kuwa na mchepuko, jmaa aliteseka sana na kwakuwa alompenda demu alivumilia ikafikia hatua jamaa akataka kuwafumania awafanye mbaya.Nilimshauri asifanye kitu kama hicho na cku ya tukio nilimchukua nikampeleka kwenye bustan ya maua tukapiga stori ili apoteze hayo mawazo. Kwa namna alivyokuwa kazama ilifikia hatua hadi kazini akaanza kuvurunda nimekomaa sana kumshawish jamaa aachane na demu huyo japo hakuwa tayari. Mungu saidia jamaa akasikia ushaur wang akapoteza mawasiliano na dem.Chaajab ni takriban mwezi 1 leo dem akampigia simu jmaa kumtaka wakutane sehem alikuw na maongezi nyeti, jmaaa kanishirikisha nikamwambie tukamsikilize demu hakuwa na stori za maana zaid ya kumtaka jamaa amsamehe warudiane na demu yuko tayari ku-conceive ili kumwamknisha kuwa kabadirika sasa wanajamvi tusaidiane kumshauri ndugu yetu nin afanye?