Kama unataka mti bora wa kivuli (majani mengi na mapana sana), matunda, mandhari mazuri (pambo), kuzuia upepo mkali na vumbi pamoja na kushikilia ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo, mkungu ndio mti sahihi.
Unakunywa maji mengi na kuzuia pia uwepo wa vinamasi na magugu.
Faida ziko maridhawa. Mengine ni tibasili kwa kutumia majani, kokwa, maua, magome na miziz yake.
Wengi hawajui kutofautisha mtiki na mkungu.