MTAZAMO: Serikali ya awamu hii ya tano, Imejawa sana hofu!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Sijui kwa nini, Ila kuna viashiria vingi vinavyoonesha kuwa serikali yetu ya awamu ya tano, au kama inavyoitwa, Serikali ya Magufuli, inajijenga katika mazingira ya hofu katika uendeshaji wa shughuli zake.

Viashiria hivyo ni pamoja na:-

1) Ubinywaji wa hali ya juu wa shughuli za upinzani nchini.

2) Uchukuaji hatua zinazoitwa za "kuwajibisha watumishi wa umma" bila kufuata sheria (no right to be heard).

3) Kuminya mamlaka wa bunge (Parliamentary Supremacy).

4) Matumizi makubwa na yasiyo ya lazima ya vyombo vya dola na visingizio mbalimbali dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa Serikali.

5) Ziara za makanisani/taasisi za dini, kutafuta credibility katika eneo hilo.

6) Watumishi wa umma sasa wanatenda kazi kwa hofu, na hivyo creativity ya uwezo binafsi unashuka siku kwa siku.

7) Serikali kuchukia sana kukosolewa na kupenda sana kusifiwa.
NAKADHALIKA.

Hofu ni adui mkubwa sana wa Ufanisi; Wazungu wana msemo wao maarufu usemao :
"The only thing to fear is fear itself".

Mungu Ilinde Tanzania.
 
Inawezekana kuna jambo umeliona ambalo wengi hawajaliona!
 
Haya yote chanzo chake ni kuwa na mtu ambaye hakuwa na sifa ya kuiongoza nchi na hajiamini hata chembe. Na ushahidi wa kutojiamini ni ubakaji wa demokrasi nchini ambao unazidi kukithiri siku hata siku na kauli zake za kujutia kuchukua form ya Urais na kutaka kurudi kwao ili akachunge ndege.

Ubakaji demokrasi nchini wa kiwango kikubwa namna hii ungekuwa rahisi miaka ya 1970s lakini si 2016. Hali ya ubakaji demokrasi kwa kiwango cha kutisha kiasi hiki kama itaendelea basi kwa mara ya kwanza Tanzania itapitia kipindi kigumu sana ambacho hakijawahi kutokea nchini tangu Tanganyika ipate uhuru miaka 55 iliyopita.
 
Anawaabisha hata wateule wake na kuwasema mpaka wazee na ccm wenzake, hili linanipa wasiwasi sana kama tutaenda salama
 
Back
Top Bottom