Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Watu wengi hasa Graduates wanavyeti vizuri na elimu zao lakini hawapati kazi!! Moja ya sababu ni kutojua kama njia anayopitia Shomari Kapombe hata wao pengine ingeweza kuwasaidia.
Kama umesoma IFM andika barua nyingi tu za maombi ya kujitolea CRDB,CBA, na sehemu nyingine bila malipo yoyote.Utaitwa tu,nenda kafanye kazi bure na baadae nenda sehemu nyingine kafanye bure ila kwa kiwango na kujituma kwa hali ya juu.
Trust me,siku ukiomba kazi NBC na kuambanisha CV yako kwamba umewahi pitia CBA na CRDB n.k uwezekano ni mkubwa sana wa wewe kuajiriwa.
Twende kwenye point,Kapombe ni mchezaji wa Simba Club kubwa na pia ni mchezaji kwa timu ya Taifa.kwenda timu ya daraja la 4,huenda wengi mkabeza ila kwangu mimi naona kama amezidi kulikaribia soko.
Pale alipo yuko sokoni,yuko kwenye matangazo ni rahisi sana kutoka Daraja la 4 kwenda la 2 na hata ligi kuu kabisa kuliko kubaki Bongo ambako msimu ukiisha,wachezaji wanakwenda kwenye "ndondo"
kwanza wachezaji wa Bongo hawana matunzo ya professional Footballers na ndiyo maana hawakawii kuchuja.Kapombe kama atajituma na kuelewa kwamba As Cannes ni sehemu ya mpito kwake,kuna siku watu watamuelewa tu.
Tatizo lenu mmekalia majungu na kuombeana mabaya ili ashindwe mje mumcheke na vimagazeti vyenu na Blog uchwara.Ndiyo maana hata timu yetu ya Taifa inafungwa ni kwa sababu tunaamini tuko daraja la kwanza,kumbe sisi tuko la nne.
Lazima tujitambue uwezo wetu