Mkuu wa Mkoa ambaye si mtendaji mtaalamu ndani ya serikali, ni mwanasiasa na kada wa CCM tu, ati anawashusha vyeo Walimu Wakuu 63. Huku mitaani watu tunashangilia, hivi tunajua madhara yake?
Elimu yetu imekosa maana na inachezewa wanasiasa watakavyo. Kwa hizi shule za Mtwara ambazo watoto hata vyoo hawana, madawati ni mtihani, walimu wanaishi kwenye vibanda wazi!
Mwalimu Mkuu ndiye sababu ya matokeo mabaya? Kwa nini Mkuu wa Mkoa asijifukuzishe kazi yeye mwenyewe, kwa mkoa wake kuwa mkiani kitaifa? Na kwa nini asishushwe cheo yeye kwa kushindwa kuisimamia idara ya elimu.
Kwa nini BURDEN ya Mtwara kufanya vibaya wapewe walimu wakuu tu? Kwa wale waliosoma Shule mbalimbali hebu wekeni uzoefu wenu hapa, hivi kweli shule hufelisha wanafunzi sababu kuu ikiwa Mwalimu Mkuu asiyetimiza wajibu wake?
Au zipo sababu nyingi na muhimu zaidi kuliko hiyo? Na mimi najiuliza na kutafakari, hivi Mkuu wa Mkoa ndiye Mwajiri wa Walimu? Hivi Mkuu wa Mkoa ndiye mpimaji na mtathmini wa elimu mkoani?
Kwanini nchi inawaachia wanasiasa wasimamie masuala ya kitaalamu kisiasa?
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].