Mtanzania aibuka kidedea huko Marekani

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,948
Aliyesimama katikati pichani ni Mtanzania kwa jina la George Jonas Mwanjisya akiwa anapokea tuzo mbele ya Balozi wa Tanzania nchini Marekani (Balozi Masilingi) mwezi huu wiki iliyopita. George alishinda "Tuzo ya Wanasayansi Weusi wenye Mchango Mkubwa Nchini Marekani". George Jonas ni Mtanzania wa Kabila la Kinyakyusa anayeshiriki katika utengenezaji wa Ndege katika kiwanda cha Boeing kilichoko Marekani, na moja ya ndege alizoshiriki katika kuzitengeneza ni ndege aina ya "Boeing 787 Dreamliner" iliyonunuliwa na Serikali yetu yaTanzania mwaka jana (2018).

George Jonas alizaliwa mwaka 1977, akiwa mtoto wa Mzee Laban Mwanjisya. George yeye alisoma elimu ya Shule ya msingi Ubungo NHC mwaka 1985 hadi 1991 na kisha kujiunga na Shule ya Sekondari ya Azania ya mjini Dar es Salaam kwa elimu ya sekondari. Baadaye alijiunga na shule ya Ilboru Sekondari ya Arusha kwa masomo ya Kidato cha Tano na Sita akichukua masomo ya mchepuo wa Physics, Chemistry na Adv. Mathematics (PCM).

Akiwa masomoni huko Ilboru sekondari, alipata nafasi ya kufanya kazi ya muda ya miezi mitatu nchini Marekani baada ya kukutana na wamarekani waliokuwa wakitafuta vijana wenye vipaji na ndoto kubwa wanaoweza kufanya kazi za muda nchini Marekani. Akiwa nchini Marekani aliomba nafasi ya kujiunga na Chuo cha Wichita (Wichita University) ambako alikubaliwa na kuchukua masomo ya Uhandisi wa Umeme na Elektroniki pamoja na Hesabu.

Baada ya safari ndefu ya masomo, mwaka 2005 aliajiriwa katika kiwanda cha Bombardier nchini Canada, ambako alifanya kazi hadi mwaka 2011. Kisha alirudi Marekani mwaka huo baada ya kupata nafasi aliyoomba katika kiwanda cha Boeing. George ameajiriwa na Boeing kama mhandisi wa umeme, na Mwaka 2015 alirudi shule katika Chuo Kikuu cha Washington (WAashington University) kwa ajili ya masomo ya Degree ya Uzamili katika Uhandisi wa Umeme.

George kwa hapa kwetu nchini Tanzania ana mradi unaojulikana kwa jina la STEM, ambacho ni kifupi cha Science, Technology, Engineering and Mathematics (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu) wenye lengo la kuongeza ushiriki wa wanafunzi katika masomo au maeneo hayo ya Sayansi.

Kwa stori na simulizi nyingi za Watanzania wenye asili ya kabila la Wanyakyusa waliowahi kuwa na umashuhuri na walio mashuhuri mpaka sasa kwenye nyanja za kitaaluma, kiuchumi, kijamii, kisiasa na umaarufu wa aina nyingine yoyote (popote pale duniani), habari zao zitakujia kupitia Kitabu cha "WANYAKYUSA MASHUHURI" ambacho bado ningali ninakiandaa. Kikiwa tayari tutajuzana!!

@ Lusako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwanda ni kosa la jinai kumtaja mtu kwa kabila lake, sijui Tanzania inaelekea wapi na huu ukabila wakati wengine ndio wamepevuka kuachana na ukabila sisi tulioacha zamani mambo hayo ndio tuinaingia. Shame
 
Ungesema Mtanzania ingetosha sana.
Viva Tanzania#
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…