Mtani kanitumia zawadi kati ya walizopewa na JF lakini nahisi nimepigwa

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,965
28,455
Wakuu,

Nafurahi leo mtani wangu kikabila [mention]GENTAMYCINE [/mention] ameweza kunitumia zawadi, maana baada ya ushindi wa JamiiForums majuzi, nilimuomba walau akipata zawadi anitumie kidogo.

Sasa kisa kinaanza alikubali atafanya hivo lakini ni wazi nimepigwa. Boksi moja kaweka jezi na skafu za timu yake ya Simba huku akijua mimi ni Yanga, na bila aibu kaweka na skafu ya simba sawa nimepokea.

Kwenye kifungashio kaniwekea jezi ya ihefu ambayo ni full, halafu kaniwekea na yeboyebo za kijani, sawa nimepokea.

Baadae kaniuliza kama nimepokea nilivojibu nimepokea amekata simu haraka sana.

Sasa nauliza hivi hii ni haki kweli? Yeye achukue mamilioni mimi niambulie yeboyebo kweli?

Naendelea kufuatilia ili nijue mwisho wake na inaonekana zawadi zenyewe kanunua Mbagala tu maana hazina kiwango kwahiyo nahisi nimepigwa mchana kweupe,
 
Screenshot_20230212-102257_Quora.jpg

Mtani katika ubora wako
 
Back
Top Bottom