MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
Wale mlio karibu na huyu mtangazaji wa Clouds tv Kipindi cha 360 Samuel Nathaniel Sasali a.k.a Emolo tafadhalini hebu jaribuni kumtafutia Kazi kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwani kwa siku za hivi karibuni amekuwa akionyesha mahaba yake ya wazi kabisa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda.
Mtangazaji huyu kila anapokuwa anasoma habari iwe chanya au hasi inayomuhusu Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam yeye amekuwa akiwa mtetezi na msemaji wake namba moja kiasi kwamba anatumia muda mwingi kuwananga wale wote wanaompinga Paul C. Makonda kitu ambacho Kiuweledi hakitakiwi kufanywa na mtangazaji wa mfano wake.
Moja ya kauli yake ambayo ameitoa leo asubuhi akiwa mubashara kabisa katika Kipindi ni kama hii ninayoinukuu hapa...." hakuna kitu kibaya kama Watu mnakesha katika mitandao kila uchao halafu mwenzenu mwanamume anazidi tu kufanya kazi na kula bata huku nyie umasikini ukiwatawala na hamtakuja hata kuthubutu kuyafikia mafanikio yake " mwisho wa kumnukuu.
Nimwombe tu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda kama anaweza ampe Kazi ya Usemaji ya Ofisi yake huyu Mtangazaji Samuel Nathaniel Sasali a.k.a Emolo kwani yawezekana pale alipo Clouds Media Group siyo mahala pake na anapoteza tu muda au akishindwa kumpa hiyo kazi basi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Makonda anaweza tu akaamua akawa anaandamana nae katika gari lake kila aendako na akampa hata kazi ya kumlinda akiwa nyumbani kwake pale pande za Oyster bay.