Mtandao wa TTCL umeniharibia siku yangu

Mtandao wa TTCL umeniharibia siku yangu

roselyn2

Member
Joined
Jun 7, 2022
Posts
86
Reaction score
390
Walichokifanya hawa watu jaman

Nimeweka salio la 500 nijiunge MB wakasema siwezi unganishwa, kuuliza salio naambiwa una 481 Tsh. Hapo sijampigia mtu, sijawasha data. Sasa hiyo kazi ya kusafiri maili mia kufuata vocha zao niitoe wapi

Nimejaribu Bufee, eti MB za 480 Tsh ni 175, halafu MB zenyewe ni zile za kubabaisha ambazo ukiamka kesho asubuhi unakuta zishakwisha hata kama hukutumia hata kidogo

Kwa sasa, ile bufee tuliokuwa tunapata MB 400 kwa 500Tsh, kwa sasa ni 200MB. Halafu kasi yake ni 2G, Picha linaanza inatumia dk nzima kufungua app ya JamiiForums. Kwa kuwa wameanza kututoza tozo hadi kwenye mtandao wao, kuanzia kesho nikitumia TTCL, naombwa nilimwe ban

Mtandao wa ovyo sana TTCL Customer Care ,bora nibaki na mtandao mmoja tu wa vodacom

Mods, acheni huu uzi uelee elee ili wayaone madhaifu yangu kwa urahisi, msiuunge kuleView attachment 2355964
Screenshot_20220913-213035.jpg
 
Ila kama uchumi sio Tatizo, mitandao ni Voda Tigo na Airtel.

Huku Halotel TTCL sijui nn hamna kitu. Janja janja tu.
 
Bufee mwanzo walikuwa wanatoa GB 10 kwa 7k..

Eti leo hii hizo 10GB wamepandisha mpaka 25k😂😂😂.... Hiki si kituko?

IMG_20220913_222804.jpg
 
Tupa laini Mzee,
Nakumbuka tulikuwa tunapata GB10 Kwa buku1 Kwa usiku.
Hata siamini nini kilitokea aisee.
Hii inchi inatuumiza SS wananchi masikini
 
Walichokifanya hawa watu jaman

Nimeweka salio la 500 nijiunge MB wakasema siwezi unganishwa, kuuliza salio naambiwa una 481 Tsh. Hapo sijampigia mtu, sijawasha data. Sasa hiyo kazi ya kusafiri maili mia kufuata vocha zao niitoe wapi

Nimejaribu Bufee, eti MB za 480 Tsh ni 175, halafu MB zenyewe ni zile za kubabaisha ambazo ukiamka kesho asubuhi unakuta zishakwisha hata kama hukutumia hata kidogo

Kwa sasa, ile bufee tuliokuwa tunapata MB 400 kwa 500Tsh, kwa sasa ni 200MB. Halafu kasi yake ni 2G, Picha linaanza inatumia dk nzima kufungua app ya JamiiForums. Kwa kuwa wameanza kututoza tozo hadi kwenye mtandao wao, kuanzia kesho nikitumia TTCL, naombwa nilimwe ban

Mtandao wa ovyo sana TTCL Customer Care ,bora nibaki na mtandao mmoja tu wa vodacom

Mods, acheni huu uzi uelee elee ili wayaone madhaifu yangu kwa urahisi, msiuunge kuleView attachment 2355964View attachment 2355965
Nawe unalalamika hiyo nusu buku na unakuja kutujazia server bure huku,wenzako tunawaza Tozo na umeme wewe unatukimbiza na hiyo mia tano.
 
Unaweza kununua vocha za TTCL kwa M pesa, sio lazima utembee sana.
 
Ila kama uchumi sio Tatizo, mitandao ni Voda Tigo na Airtel.

Huku Halotel TTCL sijui nn hamna kitu. Janja janja tu.
Tigo pia mamaamina zao tu, unajiunga kifurushi kwa matumizi yako ila wanakulazimisha sehemu itumike kusikiliza mziki 'boomplay'….. mamamaee zao!
DBA95D6B-3EE5-44BA-BDFE-CF7B93FF371C.jpeg
 
Mengine sawa walaumu ila kwenye speed mh! Hebu jaribu kuangalia na setting za simu yako pia!. Salio kukatwa lazima kutakuwa na majibu wapigie kwanza acha lawama tu!
 
Tigo hiyo jero baada ya kama wiki moja huwatabakisha hata senti na hujaifanyia huduma yoyote.
 
Mimi Halotel waliowahi kunifanyia hivyo.
Hata mimi halotel walikata pesa yangu bila ya kujiunga kitu chochote wakati sija toa ruhusa ya kukatwa bila ya kujiunga
 
Bufee mwanzo walikuwa wanatoa GB 10 kwa 7k..

Eti leo hii hizo 10GB wamepandisha mpaka 25k.... Hiki si kituko?

View attachment 2355981
Waarabu wanafanya ujuma kwenye hiyo kampuni wakishirikiana na viongozi wa ttcl na ccm lengo likiwa ni kuingia kwenye mikataba ya kifisadi kwa kisingizio kuwa ttcl ni mzingo
 
Kama kuna mtandao sijawahi kufikiria hata kwa bahati mbaya kutumia basi ni huu.
 
Ttcl ni mtandso ambao wangekuwa serious wangekuwa wakubwa kuliko mtandao wowote tz, ila sasa, ni majanga yaliyopitiliza. Nilijiunga na kifurushi cha Mb cha mwezi wakaenda offline for 2 weeks, yaani hakina jata mnata unaonekana, ikabidi nijiunge na mtandao mwingine maana muda juo wote nilikuwa sipatikani hewani, two weeks na sijui walirudi hewani lini maana nilihama mtandso wao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom