mtoto wa kibopa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 5,364
- 6,488
Hii ni hatari kwa mwenzangu na mimi asiye jus kusoma si kila siku ataliwa pesa yake hapa au mtu ambaye wa kupuuzia sms naye atalia huu ni wizi.mimi nilikuwa kila nikiacha hela nakatwa aiseeTigo wanakera balaa aisee...TCRA wamulike huku zaidi
Hata mimi hii imenikuta sana mkuu.Hivi unaunganishwaje kwenye huduma ambayo hukuiomba?Ajabu sana.Halafu wanang'ang'ania kwa nguvu zote kwamba umejiunga,inakera sana kwa kweli.Wahusika wa huu mtandao naomba mjirekebishe kwa kweli mnatuumiza sasa wananchi wenye vipato vya chini.
Tatizo lenyewe ni huu wizi wa kuwaunganisha wateja wenu vifurushi bila wahusika kujiunga yaani mkiona tu mteja amebakiza salio kwenye simu yake mtafanya kila njia muichukue.karibia miezi minne mimi nilikuwa nashindwa kuacha salio kwenye simu yangu kwa hofu ya kukatwa salio langu kila nikiwapigia tigo wanadai nitakuwa nimejiunga kifurushi ukweli sijawahi jiunga na hivo vifurushi vyao vya ajabu ajabu.juzi nikawapigia tena ndipo katika kuangaliangalia huko wakadai nimejiunga kifurushi cha HADITHI nusura nimtukane yule customer care.simu mda wote ninayo mwenyewe iweje nijiunge kwenye huo upuuzi?! Ukizingatia sijawahi ona hadithi yoyote kwa simu yangu.nikapunguza hasira nikamwomba anipe njia ya kujitoa kwenye huo upuuzi nikafanikiwa kujitoa jana nakuta wameniunga tena automatic huu so mtu kama haupo makini utalia kila siku.
na wana ile tabia ya kukata salio bila taarifa asee wanaboaHii ni hatari kwa mwenzangu na mimi asiye jus kusoma si kila siku ataliwa pesa yake hapa au mtu ambaye wa kupuuzia sms naye atalia huu ni wizi.mimi nilikuwa kila nikiacha hela nakatwa aisee
Yote mabovu, halotel ukiweka fedha bila kujiunga wanakuwa wanakata 50 kila siku bila kutumia.Sio tigo tu hata voda ... Alafu na ninyi halotel tunawaangalia tu ninyi jifanyeni.
Ndipo na mimi niliposhangaa hapo sasa.huu ni uhuni TCRA naomba na hili mlichunguze tunaumia kuna siku nimeweka 2000 ili nijiunge kifurushi cha kuongea nikachelewa kidogo tu nakuta washakata halafu ilikuwa ni muhimu kuongea na huyo mtu.daaah halafu wanakata bila kipimo leo hii kesho hii inategemeana umebakiza kiasi gani kwa simu yakoHata mimi hii imenikuta sana mkuu.Hivi unaunganishwaje kwenye huduma ambayo hukuiomba?Ajabu sana.Halafu wanang'ang'ania kwa nguvu zote kwamba umejiunga,inakera sana kwa kweli.