Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,285
- 33,881
Mwizukulu,historia yako inatufundisha nini
MTAA WA HAMZA MWAPACHU KWALE COUNTY, KENYA
Haya kanihadithia Juma Mwapachu uso kwa macho.
Juma Mwapachu anasema alipokuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki alikutana na Ali Mwakwere.
Ali Mwakwere ameshika nafasi nyingi katika serikali ya Kenya hadi kuwa Balozi wa Kenya Tanzania.
Ali Mwakwere bila shaka kwa kusikia hii ''Mwa,'' ''Mwa,'' akamuuliza Juma Mwapachu endapo yeye ni Mdigo.
Hapo Juma Mwapachu akampa historia nzima ya marehemu baba yake Hamza Kibwana Mwapachu na kumfahamisha kuwa alikuwa Mdigo wa kwanza kuingia Makerere kama mwanafunzi.
Ali Mwakwere akamuahidi Juma Mwapachu kuwa Hamza Mwapachu anastahili kukumbukwa na atahakikisha kuwa anapewa mtaa Kwale Mjini.
Ali Mwakwere alitimiza ahadi yake na nilipokutana na Ali Mwakwere kwenye maziko ya Juma Mwapachu Tanga alinieleza kuwa watu wa Kwale wamemuadhimisha Hamza Kibwana Mwapachu kwa kumpa mtaa.
View: https://www.youtube.com/shorts/2Qb6SIHyLwY?feature=share
Mbona imekaa personal Sana.
Uamuzi wa busara sana huo.Ndio utazidisha udugu kati ya watanzania na wakenya.Pakitokea ugomvi wowote ule utamalizwa kidugu na kirahisi tu.MTAA WA HAMZA MWAPACHU KWALE COUNTY, KENYA
Haya kanihadithia Juma Mwapachu uso kwa macho.
Juma Mwapachu anasema alipokuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki alikutana na Ali Mwakwere.
Ali Mwakwere ameshika nafasi nyingi katika serikali ya Kenya hadi kuwa Balozi wa Kenya Tanzania.
Ali Mwakwere bila shaka kwa kusikia hii ''Mwa,'' ''Mwa,'' akamuuliza Juma Mwapachu endapo yeye ni Mdigo.
Hapo Juma Mwapachu akampa historia nzima ya marehemu baba yake Hamza Kibwana Mwapachu na kumfahamisha kuwa alikuwa Mdigo wa kwanza kuingia Makerere kama mwanafunzi.
Ali Mwakwere akamuahidi Juma Mwapachu kuwa Hamza Mwapachu anastahili kukumbukwa na atahakikisha kuwa anapewa mtaa Kwale Mjini.
Ali Mwakwere alitimiza ahadi yake na nilipokutana na Ali Mwakwere kwenye maziko ya Juma Mwapachu Tanga alinieleza kuwa watu wa Kwale wamemuadhimisha Hamza Kibwana Mwapachu kwa kumpa mtaa.
View: https://www.youtube.com/shorts/2Qb6SIHyLwY?feature=share
Faida zote kwako ni lazima zimtaje Lissu.Hata mimi nmeshangaa yaani ni kaissue binafsi kasiko na tija kwa umma.
Seriously hamjui historia ya nchi na mchango wa Mzee Hamza Mwapachu? Basi hujitahidi angalau kujifunza kahistoria kadogo cha waliogombea uhuru wa nchi Hii! Aibu ilioje.Mwapachu kalifanyia nini TAIFA?
Faida zote kwako ni lazima zimtaje Lissu.
Huoni kuwa udugu wa wakenya na watanzania utaimarika kupitia kupeana majina ya maeneo kama hivyo.
Chizi...Sijaona hili lina faida gani kwetu. Hata wakimpa mji achana kijimtaa. Inasaidia nini?
Mohamed...Chizi...
Hamza Mwapachu ana mchango mkubwa katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Angalia video hii iliyotengenezwa na Heritage Center for Liberation na TBC:
View: https://youtu.be/oLkefadOoJ0?si=fD-X8yW1Q7-6L8H1
Biti...Seriously hamjui historia ya nchi na mchango wa Mzee Hamza Mwapachu? Basi hujitahidi angalau kujifunza kahistoria kadogo cha waliogombea uhuru wa nchi Hii! Aibu ilioje.
Endeleeni kubishana Yanga na Simba........